Dkt. Tedros: Heshima kwa wahudumu wa afya wa Rwanda wanavyopambana na Marburg
Listen now
Description
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani amewapongeza wahudumu wa afya wa nchini Rwanda kwa kazi kubwa wanaoyoifanya kukabiliana na ugonjwa wa Marburg. Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameeleza hisia zake hizo mwishoni mwa wiki alipofanya ziara katika vituo mbalimbali vya afya katika mji Mkuu wa nchi hiyo, Kigali. "Ninawapongeza wahudumu wa afya waliojitolea ambao wamejiweka hatarini kuokoa wenzao, na ambao wameendelea kufanya kazi licha ya hatari. Na ninaenzi wale ambao tumewapoteza." Pia Dkt. Tedros akaeleza kuwa yeye na wenzake wamefurahishwa na namna ya utoaji huduma ambayo haijawahi kutumiwa katika mlipuko ya magonjwa ya namna hii barani Afrika akitolea mfano wagonjwa wawili aliowashuhudia wakiendelea vizuri kwamba waliokolewa kwa kuwekewa mipira iliyopeleka hewa ndani ya mwili. “Tunaamini hii ni mara ya kwanza kwa wagonjwa wenye virusi vya Marburg barani Afrika kuingiziwa na kutolewa mpira wa hewa. Wagonjwa hawa wangefariki dunia katika milipuko ya hapo awali. Hii inaonesha kazi ambayo Rwanda imefanya kwa miaka mingi kuimarisha mfumo wake wa afya, kukuza uwezo wa huduma muhimu na msaada wa kuokoa maisha ambao unaweza kutumiwa katika huduma za kawaida za hospitali na katika dharura.”
More Episodes
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Geneva Uswisi kuwasikia vijna kutoka Kenya ambao wanashiriki kongamano la vijana, wakieleza kuhusu mkataba wa zama zijazo na mchango wao katika kuutekeleza mashinani mwao. Pia tunakuletea muhtasari wa habar iza Sudan, Kura ya Knesset kuhusu...
Published 10/29/24
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) leo kwa mara nyingine tena limetahadharisha kwamba bila msaada wa kibinadamu nchini Sudan, mamia ya maelfu wanaweza kufa kwa njaa.  Vita vya kikatili nchini Sudan vimesababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani, imeandika WFP katika...
Published 10/28/24