24 OKTOBA 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina mada inayotupeleka nchini Kenya kuzunguza na uongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu mada tofauti ikiwemo uwakilishi wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno HEKEMUA. Uchambuzi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) uliotolewa leo jijini New York, Marekani katika Siku ya Kimataifa ya Polio, unaonesha kwamba asilimia 85 ya watoto 541 waliokumbwa na polio duniani mwaka wa 2023 wanaishi katika nchi 31 zenye mifumo dhaifu, zinazokabiliwa na mizozo, halikadhalika zilizo hatarini.Umoja wa Mataifa ulijengwa na ulimwengu, kwa ajili ya ulimwengu, ndivyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, alivyouanza ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku ya leo ya Umoja wa Mataifa.Na leo Oktoba 24 huko Kazan nchini Urusi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amehutubia mkutano wa viongozi wa kundi la BRICS yaani Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini akisisititiza amani duniani akizitaja Gaza, Lebanon, Ukraine na Sudan, akiwaambia wajumbe wa BRICS, “tunahitaji amani nchini Sudan, huku pande zote zikinyamazisha bunduki zao na kujitolea katika njia ya kuelekea amani endelevuKatika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno HEKEMUA!  Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
More Episodes
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Geneva Uswisi kuwasikia vijna kutoka Kenya ambao wanashiriki kongamano la vijana, wakieleza kuhusu mkataba wa zama zijazo na mchango wao katika kuutekeleza mashinani mwao. Pia tunakuletea muhtasari wa habar iza Sudan, Kura ya Knesset kuhusu...
Published 10/29/24
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) leo kwa mara nyingine tena limetahadharisha kwamba bila msaada wa kibinadamu nchini Sudan, mamia ya maelfu wanaweza kufa kwa njaa.  Vita vya kikatili nchini Sudan vimesababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani, imeandika WFP katika...
Published 10/28/24