Ushindi wa mradi di wa Kipeto UN n ushindi wa wananchi wa Kajiado: Mnufaika
Listen now
Description
Kampuni ya Craftskills Wind Energy International Limited inayoendesha Mradi wa Kipeto Energy jana Siku ya Umoja wa Mataifa ilitwaa tuzo ya “Mtu Bora wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa.” Mradi wa Kipeto wa kampuni hiyo unatoa nishani ya umeme kwa kaya 250,000 katika eneo la Esilanke kaunti ya Kajiado nchini Kenya ukizalisha megawati 100 za umeme tangu 2021 ambazo zinaingizwa kwenye gridi ya taifa, lakini pia unasaidia kuwajengea wananchi nyumba bora na kuwapa huduma muhimu ya maji. Stela Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi amezungumza na mmoja wa wanaufaika wa mradi huo wa nishati ya upepo ya Kipeto kuhusu faida za mradi huo,  na anaanza kwa kujitambulisha..
More Episodes
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Geneva Uswisi kuwasikia vijna kutoka Kenya ambao wanashiriki kongamano la vijana, wakieleza kuhusu mkataba wa zama zijazo na mchango wao katika kuutekeleza mashinani mwao. Pia tunakuletea muhtasari wa habar iza Sudan, Kura ya Knesset kuhusu...
Published 10/29/24
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) leo kwa mara nyingine tena limetahadharisha kwamba bila msaada wa kibinadamu nchini Sudan, mamia ya maelfu wanaweza kufa kwa njaa.  Vita vya kikatili nchini Sudan vimesababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani, imeandika WFP katika...
Published 10/28/24