Grandi: Msaada wa haraka unahitajika DRC wakati wakimbizi wanaendelea kufungasha virago
Listen now
Description
Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wanaendelea kukimbilia Uganda kukwepa machafuko nchini mwao, huku rasilimali zikikaribia kikomo. Ameonya Kamishina mkuu wa  shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi, akiwa ziarani nchini Uganda hivi karibuni kwenye kambi inayohifadhi wakimbizi wa DRC na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuongeza msaada. Wakimbizi wanaokimbia mzozo  nchini DRC wanashuhudia matukio ya kutisha ya mauaji na ubakaji amesema Grandi, alipotembelea kambi ya ......aliyetembelea kambi za wakimbizi, Uganda na kusimuliwa hadithi za uchungu mkubwa “Sijawahi kusikia simulizi za machungu na hofu kama hizi za mauaji, ubakaji wa watoto mbele ya mama zao, wanawake wajawazito kukatwa vipande na makundi yenye silaha, na hofu kutawala maeneo yote ya Mashariki mwa Congo.” Kutokana na hali hii, Grandi anasema amani ndiyo inahitajika zaidi kwa sasa ili kumaliza dhuluma zinazowakumba wakimbizi wa Congo. “Ni wakati sasa jamii ya kimataifa ijitolee kwa dhati kusaidia Congo kutoka kwenye hali hii. Nilifanya kazi kama afisa wa eneo zaidi ya miaka 30 iliyopita Mashariki mwa Congo, na hali haijabadilika kimsingi.” Uganda inahifadhi jumla ya wakimbizi...... wengi wakiwa kutoka DRC, Sudan na Sudan Kusini.
More Episodes
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Geneva Uswisi kuwasikia vijna kutoka Kenya ambao wanashiriki kongamano la vijana, wakieleza kuhusu mkataba wa zama zijazo na mchango wao katika kuutekeleza mashinani mwao. Pia tunakuletea muhtasari wa habar iza Sudan, Kura ya Knesset kuhusu...
Published 10/29/24
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) leo kwa mara nyingine tena limetahadharisha kwamba bila msaada wa kibinadamu nchini Sudan, mamia ya maelfu wanaweza kufa kwa njaa.  Vita vya kikatili nchini Sudan vimesababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani, imeandika WFP katika...
Published 10/28/24