Description
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na ujumbe wa Filippo Grandi wa UNHCH ambaye yuko ziarani Uganda. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini DRC, kulikoni?
Hali Gaza inaendelea kuwa tete wakati ucheleweshwji wa kuhamisha wagonjwa hususan watoto wanaohitaji msaada wa haraka wa huduma za afya imekuwa ni hukumu ya kifo kwao huku maelfu ya watu wakiendelea kukosa mahitaji ya muhimu ya kila siku ikiwemo chakula kama mkate, yameonya leo mashirika ya Umoja wa Mataifa.Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wanaendelea kukimbilia Uganda kukwepa machafuko nchini mwao, huku rasilimali zikikaribia kikomo. Ameonya Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi, akiwa ziarani nchini Uganda hivi karibuni kwenye kambi inayohifadhi wakimbizi wa DRC na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuongeza msaada, kama inavyoeleza taarifa ya Bosco Cosmas.Makala inayotupeleka Nairobi Kenya kwake Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi akizungumza na mmoja wa wanaufaika wa mradi wa nishati ya upepo ya Kipeto Energy unaoendeshwa na kampuni ya Craftskills Wind Energy International Limited ambayo jana Siku ya Umoja wa Mataifa ilitwaa tuzo ya “Mtu Bora wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa” inayotolewa kila mwaka.Mashinani leo tutaelekea Beni, Kivu Kaskazini kusikia jinsi MONUSCO unavyowasaidia wanawake walio katika mazingira magumu, mmoja wao ni Salome Tatsopa ambaye ni mnufaika wa masomo ya ufundi wa cherahani akitueleza matumani yake baada ya mafunzo hayo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Geneva Uswisi kuwasikia vijna kutoka Kenya ambao wanashiriki kongamano la vijana, wakieleza kuhusu mkataba wa zama zijazo na mchango wao katika kuutekeleza mashinani mwao. Pia tunakuletea muhtasari wa habar iza Sudan, Kura ya Knesset kuhusu...
Published 10/29/24
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) leo kwa mara nyingine tena limetahadharisha kwamba bila msaada wa kibinadamu nchini Sudan, mamia ya maelfu wanaweza kufa kwa njaa.
Vita vya kikatili nchini Sudan vimesababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani, imeandika WFP katika...
Published 10/28/24