Description
Hii leo jaridani tunaangazia janga la nja linalokumba wananchi waathirika wa mizozo nchini Sudan, na simulizi za walinda amani wa UNIFIL nchini Lebanon. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Haiti, kulikoni?
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) leo kwa mara nyingine tena limetahadharisha kwamba bila msaada wa kibinadamu nchini Sudan, mamia ya maelfu wanaweza kufa kwa njaa.Kikosi cha muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL, ambapo, katikati ya mvutano unaoongezeka kati ya Lebanon na Israel, walinda amani walioko katika makao makuu ya UNIFIL huko Naqoura wamekuwa wakivumilia mazingira magumu. Ushuhuda wa hivi karibuni kutoka kwa walinda amani hao unaonesha ukubwa wa changamoto wanazokabiliana nazo, ikiwemo vitisho vilivyoongezeka kutoka kwa shughuli za kijeshi za Israel zilizo karibu na eneo hilo, vizuizi vya kusafiri, na changamoto za uendeshaji wa shughuli.Makala inatupeleka Nairobi Kenya kwa washindi waliotwaa tuzo ya “Mtu Bora wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa 2024” ambao ni kampuni ya Craftskills Wind Energy International Limited wamiliki wa mradi wa nishati ya upepo ya Kipeto Energy iliyoko Kaunti ya Kajiado nchini Kenya.Katika mashinani mashinani leo tutakuwa Haiti ambapo nafasi ni yake Andre Rose, mama wa kijana Kerby, akieleza jinsi msaada wa kifedha unaotolewa na Shirika la UNICEF umekuwa mkombozi kwa familia yake iliyolazimika kukimbia makazi yao kutokana na ghasia za magenge ya uhalifu nchini Haiti.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Geneva Uswisi kuwasikia vijna kutoka Kenya ambao wanashiriki kongamano la vijana, wakieleza kuhusu mkataba wa zama zijazo na mchango wao katika kuutekeleza mashinani mwao. Pia tunakuletea muhtasari wa habar iza Sudan, Kura ya Knesset kuhusu...
Published 10/29/24
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) leo kwa mara nyingine tena limetahadharisha kwamba bila msaada wa kibinadamu nchini Sudan, mamia ya maelfu wanaweza kufa kwa njaa.
Vita vya kikatili nchini Sudan vimesababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani, imeandika WFP katika...
Published 10/28/24