Description
NASIKIA KUITWA.
I Hear Thy Welcome Voice.
Na, Lewis Hartsough 1828 - 1919.
Lewis Hartsough alizaliwa Agosti 31, 1828, Ithaca, New York Marekani na alihitimu masomo yake huko Cazenovia Seminary mwaka 1852. Aliwekwa wakfu kuwa Mtumishi wa ki-methodist [Methodist Minister] mwaka 1853, na alijiunga na Oneida Conference ya New York Marekani. Yapata mwaka 1868, alihamia magharibi mwa nchi kwa sababu za kiafya, ambapo alikujakuwa mwangalizi mkuu wa the Utah Mission, baadaye mzee mwangalizi wa the Wyoming District. Katika kipindi hicho hicho alitumika kama Mhariri wa muziki wa Joseph Hillman’s Revivalist. Mnamo mwaka 1871, Lewis Hartsough alisimikwa kuwa Pastor wa Methodist church huko Epworth, Iowa. Alihamia Northwest Iowa Conference mwaka 1874, na kustaafu mwaka 1895. Roho yake ilitwaliwa Mbinguni Januari 1, 1919 na mwili wake kuhifadhiwa huko Mount Vernon, Iowa Marekani.
“Nasikia Kuitwa” uliotungwa mwaka 1872 na mpaka sasa ambapo kitabu hiki kinakuijia umelihudumia Kanisa kwa miaka ipatayo 143, ni wimbo ambao wakati wowote uwao ule unapoimbwa basi kila muamini katika Kristo aliye hai, anapata msisimko unaoalika uwepo wa ajabu sana na kupelekea kuzama katika kumtafakari Kristo katika hali ya Rohoni zaidi. Wimbo huu ni kati ya nyimbo za Tenzi zinazopendeka sana miongoni mwa Wakristo wanaouchukulia utume mkuu wa YESU Kristo duniani kwa namna ya kipekee sana.
Asili na muktadha wa wimbo huu vinaegemea katika ukombozi wa msalaba na kuuhishwa kwa njia ya damu ya thamani ambapo dhambi/taka zinasafishwa na unyonge unabadilishwa na nguvu mpya ya upendo, imani na tumaini la Mbinguni. Ni wimbo ambao umemtangazia shetani waziwazi kushindwa kwake na mioyo yetu ya imani inashuhudiwa hivyo na kwamba zipo ahadi, haki na nguvu ndani ya wokovu wetu kama tukiamini.
Ujumbe wa “Nasikia Kuitwa” wa Pastor Lewis, unadhihirisha kama vile alikuwa katika uhitaji [labda kutokana na afya yake na huduma yake] ambapo baada ya kuzama katika kuutafuta uso wa MUNGU akasikia sauti ikimwita apasogelee msalaba kwa ajili ya utakaso kwa njia ya damu ya YESU.
Mimi na wewe ni mara ngapi tuwapo katika utumishi wetu na labda katika hali ya kuhitaji tumetulia mbele za MUNGU kwa ajili ya kusikia sauti yake? Tunaweza kuleta hesabu zetu mezani kuthibitisha madai haya?