SHUHUDA ZA TENZI na Emmanuel Shedo
Listen now
Description
BW MUNGU NASHANGAA KABISA. How Great Thou Art. Tenzi 114.                                      Na, Stuart Keene Hine 1899 - 1989. Bw. MUNGU Nashangaa Kabisa! Umechaguliwa na wapenzi wa nyimbo za sifa huko Great Britain, kuwa utenzi wa Rohoni unaotumika kwenye hafla nyingi nchini humo. Nchini Marekani “Bw. MUNGU Nashangaa Kabisa!” ulirekodiwa na Elvis Presley na wasanii wengine wengi. Ulikuja kuwa sauti kuu [main vocal] iliyotumika kwenye matangazo ya kipindi cha kila wiki cha Billy Graham’s Hour of Decision [Saa ya uamuzi ya Billy Graham] na ulijipatia tuzo mbili za Grammy. Stuart aliguswa kuandika utenzi wake ndani ya miaka 14 na kwa mara ya kwanza kuuingiza katika jarida lake la Injili lililojulikana kwa jina la Grace and Peace [Neema na Amani] la tarehe 15 Aprili 1949. Mguso wake kwa wimbo huu ulitokana na uzoefu wake mwenyewe alioupitia katika milima ya Carpathian na kusikiliza kutoka utenzi wa Ivan Prokhanoff Mwana-utenzi wa Kirusi aliyeghani wimbo wake wa Mungu mwenye nguvu [Mighty God] ambao aliuegemeza kwenye shairi la Carl Boberg la “O Store Gud”. Stuart Keene Hine alizaliwa Magharibi mwa London mnamo tarehe 25 Julai 1899, kama mvurugano vile, karne mpya ilikaribia. Alikata shauri mwenyewe kwa ajili ya Kristo katika umri wa miaka 14 na muda mfupi baadaye alibatizwa. Katika umri wa miaka 18, Stuart aliitwa kwa ajili ya utumishi katika jeshi nchini Ufaransa. Hizi zilikuwa siku za utisho, lakini imani ya Mtumishi wa MUNGU Stuart ilibaki kuwa imara. Akirudi London disemba 1919, Stuart mwishowe alipata ajira kama karani katika kampuni ya kimataifa ya Kijapani ya Mitsubishi. Yapata mnamo 20 Juni 1923, katika Kanisa la Manor Park Baptist Church, Mtumishi wa MUNGU Stuart alimuoa Mercy Salmon na ndani ya mwezi mmoja tu wa ndoa yao waliamua kwenda Poland kuanza kipindi cha utumishi katika Ulaya Mashariki ambao ulikuwa ukamilike kwa zaidi ya miaka 16. Mnamo mwezi Juni 1934 Mtumishi Stuart alianza safari ya umissioni ya maili 300 kwa baiskeli kuwafikia watu wa viunga vya Carpathian Mountains, ebu fikiria ni muda gani ingemgharimu. Ni safari hii ndiyo ilizaa utenzi wake wa “Bw. MUNGU Nashangaa Kabisa!” Akiwa njiani aliona jinsi ya mandhari maridadi ya uumbaji wa MUNGU katika ile milima, galaksi za angani, viumbe vilivyomo katika ile milima, uvumi wa mito, milio ya ndege wa angani na wanyama, uvumi wa miti wakati upepo unapovuma “Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo, na miti yote ya kondeni itapiga makofi Isa.55:12”, akavutiwa Rohoni sana na ukuu, uweza, mamlaka na nguvu za MUNGU.  Hata wewe na mimi ni kazi ya mikono toshelevu ya MUNGU na ametuumba kwa jinsi ya ajabu pia, wewe na mimi tuna hazina ya kipekee ambayo haikuwahi kuwepo duniani na huenda isiwepo tena, mshukuru MUNGU kwa jinsi ulivyo kwa maana kuna mtu akikuona anakutamani jinsi ulivyo na kusema moyoni mwake hakika huyu amebarikiwa, hakika MUNGU unanishangaza sana kwa jinsi ulivyomuumba huyu ninayemuona hivi sasa!. Kuna watu wengine hawaoni utu wako wa nje lakini wanaona utu wako wa ndani na kuutamani sana jinsi ulivyo. Ukitaka pia kutafakari ukuu wa MUNGU ebu fikiria zile galaksi [nyota za angani] ambazo hadi sasa kwa mujibu wa wanajimu zimegunduliwa zaidi ya milioni 300 [ugunduzi unaendelea] ambazo ni kubwa na nzito kuliko sayari ya dunia hii tunayoishi na zinaelea tu huko anga za juu [space] bila ya nguzo iliyozishika na ajabu zaidi ni pale zinapojizungusha na kulizunguka jua pasina kukosea njia zao [bila kugongana] hata kidogo tangu uumbwaji wao, huku tukiambiwa kuwa kwa ukubwa na uzito wao, moja tu ikidondokea dunia hii tunayoishi basi itasambaratishwa kabisa na mahala pake pasijulikane asilani! Lakini ebu ona jinsi ambavyo zinatii amri na uweza wa NENO la MUNGU iliyoziweka huko. Kwa tafakari hii kwa nini tusimshangae MUNGU kabisa kama ambavyo Mtumishi Stuart alivyomshangaa.
More Episodes
NASIKIA KUITWA. I Hear Thy Welcome Voice. Na, Lewis Hartsough 1828 - 1919. Lewis Hartsough alizaliwa Agosti 31, 1828, Ithaca, New York Marekani na alihitimu masomo yake huko Cazenovia Seminary mwaka 1852. Aliwekwa wakfu kuwa Mtumishi wa ki-methodist [Methodist Minister] mwaka 1853, na...
Published 12/29/20
Maneno ya Wimbo yametungwa na Horratio gates Spaffod na Sauti tune ni Philip P. Bliss waimbaji ni kwaya ya Gospel Kijenge Arusha Tanzania East Africa
Published 09/18/20