19 JANUARI 2023
Listen now
Description
Hii leo jaridani tuna habari kwa ufupi, mada kwa kina na jifunze lugha ya kiswahili. Katika Habari kwa Ufupi na Leah Mushi: Kuelekea siku ya kimataifa ya elimu tarehe 24 Januari, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO Bi. Audrey Azoulay, amesema ametoa heshima ya siku hiyo kuwa maalum kwa wanawake na wasichana wa Afghanistan ambao mamlaka ya Taliban imewanyima fursa ya kupata elimu. Mahakama nchini Afrika Kusini imewaruhusu wataalamu wa Umoja wa Mataifa kushiriki kwenye kesi iliyofunguliwa na wananchi wa wilaya ya Kambwe nchini Zambia walioathirika na uchimbaji wa madini uliofanywa na Kampuni ya madini ya Anglo Amerika. Na leo ni siku ya mwaka mpya wa Kichina ambapo kwa mujibu wa kalenda ya nchi hiyo ni mwaka wa Sungura. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametuma salamu za mwaka mpya kwa taifa hilo na kulishukuru kwa ushirikiano wake linaoutoa kwa Umoja wa Mataifa na dunia kwa ujumla. Na katika Mada kwa Kina tunakwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako takriban watu 233,000, wamelazimika kuyahama makazi yao katika wilaya ya Nyiragongo jimboni Kivu Kaskazini  kutokana na vita vinavyochochewa na kundi la wapiganaji waasi la M23 na sasa UNHCR imewajengea makazi badala ya kutegemea kuishi tu katika maeneo ya wazi, shuleni au makanisani. Shuhuda ni mwandishi wetu wa DRC, Byobe Malenga. Katika kujifunza lugha ya kiswahili, tunabisha hodi Baraza la Kiswahili la Taifa, Zanzibar, BAKIZA kwake Katibu Mtendaji Dkt. Mwanahija Ali Juma akifafanua methali ACHEKAYE KOVU HAJAONA JERAHA. Karibu na mwenyeji wako ni Anold Kayanda
More Episodes
Mnamo tarehe Mosi Januari mwaka 2016, Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yalianza kufanyiwa kazi rasmi. Tangu wakati huo watu ulimwenguni kote kwa ngazi tofautifauti wamekuwa wakihaha kuhakikisha kufikia mwaka 2030 malengo hayo yanafikiwa. Na kila mara Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini...
Published 05/09/24
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adili na Idili.”
Published 05/09/24