Misaada wawasili kwa mara ya kwanza katika eneo la Donetsk Oblast Ukraine: OCHA
Listen now
Description
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA limesema kwa mara ya kwanza misaada ya mashirika ya Umoja wa Mataifa imefanikiwa kuwasili katika eno linalodhibitiwa na serikali karibu na Soledar Mashariki mwa Donetsk Oblast nchini Ukraine. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswis na OCHA msaada huo wa kibinadamu uliosheheni kwenye malori matatu ni kwa ajili ya kuwasaidia zaidi ya watu 800 ambao walisalia katika jamii zinazozunguka eneo laSoledar.  “Msaada huo unaojumuisha chakula, maji, vifaa vya usafi na kujisafi, madawa na vifaa tiba vingine umetolewa na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani WHO, la kuhudumia Watoto UNICEF, la uhamiaji IOM na la mpango wa chakula duniani WFP na unaratibiwa na OCHA.”  Mashirika hayo yamesema mapigano ya hivi karibuni katika viunga vya Soledar yamesababisha uharibifu mkubwa na kuwaacha mamia ya watu kwenye eneo hilo katika hali mbaya na hivyo kutegemea msaada wa kibinadamu.  Hii ni mara ya kwanza msafara huo wa misaada wa mashirika ya kibinadamu unawasili katika eneo hilo na OCHA inasema “ Tumeziarifu mapema pande zote katika mzozo kuhusu msafara wetu kupitia mfumo wa taarifa wa masuala ya kibinadamu.”  Mashirika ya kibinadamu nchini Ukraine yakiratibiwa na OCHA yanajitahidi kuongeza idadi ya misafara ya misaada ya pamoja katika eneo hilo lililo mstari wa mbele wa mapambano nchini Ukraine ambako mahitaji ni makubwa.   OCHA inasema misafara zaidi ya misaada inatarajiwa katika siku chache zijazo. 
More Episodes
Hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII ukielekea ukingoni huku mambo kadha yakiwa yamejadiliwa kwa wiki mbili na miongoni mwa mambo hayo ni suala la mabadiliko ya tabianchi na mazingira, nilipata fursa ya kuzungumza na...
Published 04/25/24
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu leo ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya maneno “Adhimisha na Azimisha.”
Published 04/25/24