27 JANUARI 2023
Listen now
Description
Hii leo jaridani tuakuletea ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuhusu makumbusho ya Holocaust, pia tunamulika kazi ya walinda amani nchini DR Congo. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani tunasalia hapa makao makuu wa Umoja wa Mataifa. Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kumbukizi ya waathitrika wa mauaji ya maangamizi makubwa au Holocaust dhidi ya wayahudi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mauaji hayo yalikuwa ni malimbikizo ya miongo ya chuki dhidi ya Wayahudi ndio maana sasa ni wakati wa kuhakikisha chuki za aina yoyote ile zinakomeshwa duniani.Kufuatia mashambulizi yanayofanywa na makundi mbalimbali ya waasi kwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hususani mashariki mwa nchi hiyo ya pili kwa ukubwa wa eneo barani Afrika, walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha 9 kutoka Tanzania, TANZBATT 9 kinachohudumu katika kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kujibu mashambulizi cha FIB-MONUSCO, wamefanya doria katika barabara ya Mbau-Kamango nje ya mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini.Makala tunakwenda nchini Tanzania kusikia ni kwa vipi Mahakama inachagiza moja ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs na shuhuda wetu ni Hamad Rashid wa Redio washirika MVIWATA FM mkoani Morogoro, Mashariki mwa Tanzania.Katika mashinani leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kukumbuka waathirika na waliokufa kutokana na mauaji ya maangamizi dhidi ya wayahudi yaliyofanywa na manazi nakuletea ujumbe wa nini kifanyike kuepusha hali hiyo na ujumbe unatolewa na Dani Dayan, Mwenyekiti wa jumba la makumbusho ya mauaji ya maangamizi ya wayahudi huko Israel, liitwalo Yad Vashem. Ujumbe huu ameutoa wakati wa uzinduzi wa maonesho ya kitabu chenye majina ya wayahudi waliouawa na manaziMwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
More Episodes
Mnamo tarehe Mosi Januari mwaka 2016, Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yalianza kufanyiwa kazi rasmi. Tangu wakati huo watu ulimwenguni kote kwa ngazi tofautifauti wamekuwa wakihaha kuhakikisha kufikia mwaka 2030 malengo hayo yanafikiwa. Na kila mara Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini...
Published 05/09/24
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adili na Idili.”
Published 05/09/24