Maelfu ya wakimbizi wa ndani wa Tambura warejea makwao
Listen now
Description
Sudan Kusini ni moja ya nchi iliyoathirika kwa muda mrefu na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo mara kwa mara makundi ya wapiganaji wenye silaha yalikuwa yakivamia katika vijiji na kuwaua raia na kupora mali zao. Kutokana na sababu hiyo wananchi wengi wamekuwa wakikimbilia katika kambi za kijeshi zilizoko karibu na maeneo yao ili kusaka hifadhi. Lakini mazungumzo na mipango ya amani inayotelekezwa nchini humo kwa ushirikiano wa serikali, Umoja wa Mataifa na wadau wengine umeleta matunda na sasa maeneo mengi amani na utulivu umerejea. Moja ya maeneo hayo ni katika jimbo la Equotoria Magharibi ambapo maelfu ya wakimbizi waliokuwa katika kambi za wakimbizi wa ndani za eneo la Tambura kuanzia mwishoni mwa mwaka jana 2022 wameanza kurejea makwao ili kuendelea na maisha ikiwemo watoto kurejea shuleni na kuendelea na shughuli za kilimo. Tuungane na Leah Mushi katika makala hii akisimulia zaidi.
More Episodes
Mnamo tarehe Mosi Januari mwaka 2016, Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yalianza kufanyiwa kazi rasmi. Tangu wakati huo watu ulimwenguni kote kwa ngazi tofautifauti wamekuwa wakihaha kuhakikisha kufikia mwaka 2030 malengo hayo yanafikiwa. Na kila mara Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini...
Published 05/09/24
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adili na Idili.”
Published 05/09/24