27 MACHI 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunaangazia jitihada za kukomesha mlipuko wa kipindupindu uliozuka nchini Zambia, na mchango wa wasanii katika msaada wa kibinandamu nchini DRC. Makala tunamulika mgogoro ambao hauripotiwi sana kaskazini mwa Msumbiji na mashinani tunasalia nchini DRC, kulikoni? Juhudi na ushirikiano wa pamoja wa wahudumu wa afya, vituo na Jamii, vimefanikisha kukomesha mlipuko wa kipindupindu uliozuka nchini Zambia kwa mujibu wa Shirika Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO nchini Zambia, ambalo limeeleza kwamba ugunduzi wa mapema na matibabu husaidia kukabiliana na ugonjwa huo na kupunguza idadi ya vifo.Mwanamuziki Innocent Balume, al maaruf Innoss’B ametangazwa kuwa muungaji mkono wa ngazi ya juu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP katika kusongesha milo yenye afya na lishe bora nchini mwake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala tunaangazia mgogoro ambao hauripotiwi sana kaskazini mwa Msumbiji umesababisha mamia kwa maelfu ya familia kuwa wakimbizi, ambao wanaendelea kutatizika kutafuta chakula, malazi na usalama.Na mashinani tutaelekea nchini Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo DRC kusikia ujumbe wa mlinda amani wa kuhusu elimu kwa wasichana.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
More Episodes
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua totauti ya matumizi ya maneno "ELEKEZA NA ELEZA."
Published 05/02/24
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika uhuru wa vyombo vya habari ikijikita kwenye umuhimu wa uandishi wa habari na uhuru wa kujieleza katika muktadha wa kukabiliana na janga la tabianchi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno la wiki. Nchini Kenya mafuriko...
Published 05/02/24