28 MACHI 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tnakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kufuatilia jitihada za mashirika za kuhahikisha watoto waathrika wa mimba za utotoni wameweza kurejea shule. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za Gaza, Haiti na wakimbizi wakimbizi wa Sudan Kusini. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunapata maana ya neno “UDENDA.”  Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina (UNRWA) leo Machi 28 limetahadharisha kuhusu ujio wa baa la njaa katika Ukanda wa Gaza. UNRWA imesema yenyewe ni uti wa mgongo wa misaada ya kibinadamu Gaza lakini bado misafara yao ya chakula imezuiwa kufika kaskazini, ambako baa la njaa linajongea. Wakati huo huo Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limesema kati ya hospitali 36 katika Ukanda wa Gaza, ni 10 tu ambazo zimesalia zikifanya kazi japo nazo kwa kiasi kidogo.Ripoti ya Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa leo inataka hatua za haraka na za ujasiri ili kukabiliana na hali ya "janga" nchini Haiti. Ripoti imeeleza kuwa magenge yanaendelea kutumia unyanyasaji wa kingono kuwatendea unyama, kuwaadhibu na kuwadhibiti watu. Wanawake wamebakwa hata baada ya kushuhudia waume zao wakiuawa mbele yao. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), pamoja na wadau wake 123, Alhamis ya leo limetangaza kuwa linatafuta dola bilioni 1.4 mwaka huu ili kukidhi mahitaji ya wakimbizi milioni 2.3 wa Sudan Kusini wanaoishi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Ethiopia, Kenya, Sudan na Uganda. Janga la wakimbizi wa Sudan Kusini linasalia kuwa ndilo kubwa zaidi barani Afrika.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “UDENDA”.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
More Episodes
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua totauti ya matumizi ya maneno "ELEKEZA NA ELEZA."
Published 05/02/24
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika uhuru wa vyombo vya habari ikijikita kwenye umuhimu wa uandishi wa habari na uhuru wa kujieleza katika muktadha wa kukabiliana na janga la tabianchi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno la wiki. Nchini Kenya mafuriko...
Published 05/02/24