Ujumuishwaji wa wanawake katika huduma za kifedha ni muhimu - Nangi Massawe, Benki Kuu Tanzania
Listen now
Description
Lengo namba 5 la maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa au SDG5 linahimiza kila nchi kuhakikisha wanawake wanawezeshwa na kujumuishwa katika kila nyanja ya Maisha ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 hawasalii nyuma katika maendeleo. Moja ya masuala yanayotiliwa msukumo zaidi hivi sasa ni ujumuishwaji wa wanwake katika masuala ya huduma za kifedha n anchi nyingi zimeanza kuchukua hatua ikiwemo Tanzania. Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili amezungumza na Nangi Moses Massawe kutoka Benki Kuu ya Tanzania ambaye ni meneja wa kitengo cha huduma jumuishi za kifedha. 
More Episodes
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua totauti ya matumizi ya maneno "ELEKEZA NA ELEZA."
Published 05/02/24
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika uhuru wa vyombo vya habari ikijikita kwenye umuhimu wa uandishi wa habari na uhuru wa kujieleza katika muktadha wa kukabiliana na janga la tabianchi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno la wiki. Nchini Kenya mafuriko...
Published 05/02/24