Ni dhana potofu kudai Wamaasai wanaua Simba ili kupata mke - Alois Porokwa
Listen now
Description
Katika harakati za kupambana na mabadiliko ya tabianchi, kuna wakati jamii ambazo bado zinaishi kiasili zimekuwa zikilaumiwa kwamba zinachangia kuharibu mazingira kutokana na wao kuishi katika mazingira fulani; mathalani misitu na mbuga jambo ambalo linakanushwa na jamii hizo wakidai kwamba kimsingi wao ndio watunzaji wazuri wa mazingira kwani wanayategemea moja kwa moja kwa mustakabali wa maisha yao ya kila siku na siku zijazo. Hivi karibuni wakati wa Mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 uliofanyika jijini Nairobi, Kenya, Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Kenya, Stella Vuzo alimhoji Alois Porokwa, Mkurugenzi wa shirika la NALEPPO kutoka jamii ya Wamaasai aliyesafiri kutoka Kijiji cha Emboreet, Wilaya ya Simajiro, Mkoa wa Manyara, Tanzania. Ni katika mazungumzo hayo ndipo Stella Vuzo akakumbuka kumuuliza Alois Porokwa swali hili ambalo ni dhana inayohusisha jamii ya Wamaasai kuua wanyama.
More Episodes
Nchini Tanzania mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza mitaji, UNCDF uitwao CookFund unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya umesaidia wajasiriamali hasa wanawake kuinua wanawake wenzao kwenye sekta ya matumizi ya nishati jadidifu na hivyo kutekeleza ajenda ya 2030 ya Umoja wa Mataifa ya...
Published 04/29/24
Hii leo jaridani tunaangazia mzozo na hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na msaada wa kibinadamu nchini Ethiopia. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Somalia, kulikoni?  Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeonya hii leo juu ya...
Published 04/29/24