Watoa chanjo wavuka mabonde na mito kufikisha chanjo kwa walengwa Tanzania
Listen now
Description
Wiki ya kimataifa ya chanjo ikifungua pazia, nchini Tanzania wahudumu wa afya kama Prisca Mkungwa wanajitoa kwa kadri ya uwezo wao kuhakikisha huduma za chanjo zinafikia walengwa wote hata wale walioko maeneo ya mbali. Mathalani huko wilayani Chunya, mkoani Mbeya, kusini magharibi mwa taifa hilo ambako kupitia ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, chanjo dhidi ya surua inatolewa kwa watoto. Prisca na wenzake kutokana na kupenda kazi yao wanafanya kila njia iwe ni kutumia usafiri wa bodaboda au hata kuvuka mito na mabonde kwa miguu kuhakikisha chanjo zinafika. Kufahamu kwa kina ungana na Assumpta Massoi katika makala hii iliyoandaliwa na UNICEF Tanzania.
More Episodes
Leo ikiwa ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani maudhui yakiwa ni Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira, Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa akimulika sakata la vifo vya waandishi wa habari wanaoweka maisha yao rehani kuripoti masuala ya mazingira. 
Published 05/03/24
Tukiwa katika msimu wa mvua kwa nchi nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara, tuelekee nchini Somalia, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura, OCHA limesema wao na wadau wao wamejiandaa kufikisha mahitaji kwa watu 770,000 katika wilaya 22 za nchi hiyo...
Published 05/03/24