Wiki ya Chanjo Duniani yaanza leo 24 hadi 30 Aprili 
Listen now
Description
Leo ni siku ya kwanza ya siku saba za Wiki ya Chanjo Duniani. (Taarifa ya Anold Kayanda) Wiki ya Chanjo Duniani ambayo huadhimishwa katika kila wiki ya mwisho ya mwezi Aprili, inalenga kuangazia hatua za pamoja zinazohitajika na kuhimiza matumizi ya chanjo kuwalinda watu wa rika zote duniani dhidi ya magonjwa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO linashirikiana na nchi kote ulimwenguni kuhamasisha ufahamu wa thamani ya chanjo na uchanjaji na kuhakikisha kuwa serikali zinapata mwongozo unaohitajika na usaidizi wa kiufundi ili kutekeleza programu za uchanjaji zenye ubora wa hali ya juu. Lengo kuu la Wiki ya Chanjo Duniani ni kwa watu zaidi  na jamii zao kulindwa dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika. WHO inasema chanjo zimesaidia sana ikitolea mfano namna ulimwengu umeweza kutokomeza ugonjwa wa ndui ambapo mtu wa mwisho kuugua ugonjwa huo ni miaka 47 iliyopita. Mwaka huu Wiki ya Chanjo Duniani inaadhimisha miaka 50 ya EPI ambao ni mpango ambao WHO iliuanzisha mwaka 1974 kwa lengo la kufanya chanjo zipatikane kwa watoto wote duniani. WHO inatoa wito kwa nchi kote duniani kuongeza uwekezaji katika mipango ya chanjo ili kulinda vizazi vijavyo. Tags: Siku za UN, WHO, Chanjo, EPI, Wiki ya Chanjo Duniani
More Episodes
Leo ikiwa ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani maudhui yakiwa ni Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira, Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa akimulika sakata la vifo vya waandishi wa habari wanaoweka maisha yao rehani kuripoti masuala ya mazingira. 
Published 05/03/24
Tukiwa katika msimu wa mvua kwa nchi nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara, tuelekee nchini Somalia, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura, OCHA limesema wao na wadau wao wamejiandaa kufikisha mahitaji kwa watu 770,000 katika wilaya 22 za nchi hiyo...
Published 05/03/24