Raia Sudan wakumbwa na kihoro kufuatia mapigano kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa RSF
Listen now
Description
Huko nchini Sudan jimboni Darfur Kaskazini, hususan mjini El-Fasher na viunga vyake mapigano kati ya jeshi la serikali SAF na wanamgambo wa RSF yanazidi kuwa na madhara kwa rai ana kumtia hofu kubwa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk. Katika kufahamu hali iko vipi, Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Seif Magango msemaji wa ofisi ya Kamishna Türk kutoka Nairobi, Kenya na anaanza kwa kueleza nini hasa kinamtia hofu Kamishna huyo.
More Episodes
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya ambako Umoja wa mataifa uko mstari wa mbele kuwapa msaada wakenya wanaotatizika kutokana na mafuriko. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kuhusu Gaza, Uhamiaji na misitu. Mashinani inatupeleka nchi Haiti, kulikoni?  Katibu Mkuu...
Published 05/07/24
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR, linapambana kuhakikisha linawasaidia wakimbizi katika maeneo mbalimbali ya ukanda wa Afrika Mashariki dhidi ya madhila yanayosababishwa na mafuriko makubwa kutoka na mvua za El Niño zinazoendelea. Makala hii ambayo video zake zimekusanywa...
Published 05/06/24