30 APRIL 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, Adam Kulet Ole Mwarabu Ole Mareka kutoka jamii ya Wamaasai wa Parakuyo iliyoko mjini Morogoro nchini Tanzania anazungumza na Flora Nducha. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani. Kamishina Mkuu wa sririka la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA leo amesema watu waliokamatwa wakati wa vita inayoendelea Gaza wamenyanyaswa, kuteswa na kufanyiwa vitendo visivyo vya kibinadamu. Katika taarifa yake iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi Phippe Lazzarini amesema “Watu tuliozungumza nao wametueleza kwamba walipokamatwa kila mara walikuwa wakikusanywa Pamoja, kuvuliwa nguo na kubaki na chupi na kisha kupakiwa katika malori. Watu hawa wametendewa vitendo vya kikatili visivyo vya kibinadamu ikiwemo kuzamishwa kwenye maji na kuumwa na mbwa.”Jahmhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ndio nchi yenye idadi kubwa ya watu wanaohitaji msaada wa kibinadamu duniani kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada wa kibinadamu na masuala ya dharura OCHA. Katika ukurasa wake wa X hii leo shirika hilo limesema jimboni Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini pekee watu milioni 5.4 hawana uhakika wa chakula, milioni n6.4 ni wakim bizi wa ndani na wagonjwa wa kipindupindu kwa mwaka huu pekee wamefikia 8,200. OCHA imeongeza kuwa sasa dola bilioni 1.48 zinahitajika ili kutoa msaada wa kuokoa Maisha kwa watu zaidi ya milioni 4.  Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amesema anatatizwa na mlolongo wa hatua nzito zinazochukuliwa kutawanya na kusambaratisha maandamano katika vyuo vikuu mbalimbali nchini Marekani.Kupitia tarifa yake iliyotolewa leo mjini Geneva Bwana Türk amesisitiza kuwa "Uhuru wa kujieleza na haki ya kukusanyika kwa amani ni jambo la msingi kwa jamii  hasa wakati kuna kutokubaliana vikali juu ya masuala makubwa, kama vile ilivyo sasa ikihusiana na mzozo unaoendelea katika eneo la Palestina linalokaliwa na Israel,"Na katika mashinani shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP linashirikisha wadau mbalimbali katika harakati za kutunza mazingira kupitia upandaji miti na kupitia video iliyofanikishwa na washirika wetu Radio Domus FM nampisha mwanaharakati wa mazingira ambaye alitembelea eneo Bunge la Ngong katika kaunti ya Kajiado  jijini Nairobi ili kushirikiana na wanafunzi katika kutimiza wito wa UNEP wa upanzi wa miti.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
More Episodes
Makala hii inamwangazia Meja Lilian Laizer, Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa anayehudumu katika Kikosi cha 7 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR chini ya MINUSCA ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini humo. Meja...
Published 05/20/24
Kuongezeka kwa shughuli za kijeshi huko Rafah, kusini mwa Gaza, kumesababisha mamia kwa maelfu ya watu kuyahama makazi yao, na kufanya maisha kuwa magumu zaidi kwa maelfu ya familia ambazo tayari zimelazimika kuyahama makazi yao mara kadhaa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula...
Published 05/20/24