Mabadiliko ya tabianchi yamefanya urembo wa Kimaasai Kenya kuwa mbadala wa kujikimu kimaisha: Samante Anne
Listen now
Description
Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa mwiba kwa jamii nyingi yakizilazimu kubadili mfumo wao wa Maisha ili kukabiliana na athari zake kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa jamii zilizoathirika na janga hilo ni za watu wa asili wakiwemo Wamaasai kutoka Kenya na hususan wanawake. Je wanahimili vipi athari hizo? Flora Nducha alipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wanawake wa jamii hizo za Wamaasai aliyekuwa New York hivi karibuni kushiriki jukwaa la watu wa jamii za asili Bi. Samante Anne kutoka shirika lisilo la kiserikali nchini Kenya la Mainyoito Pastoralists Intergrated Development Organization (MPIDO).   
More Episodes
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatilia mradi wa mradi wa Cookfund, Elisabeth Ngoye amezungumza na Laurien Kiiza wa UNIC Dar es Salaam. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za afya, Gaza na Ukraine. Mashinani inatupeleka nchini Kenya,...
Published 05/21/24
Makala hii inamwangazia Meja Lilian Laizer, Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa anayehudumu katika Kikosi cha 7 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR chini ya MINUSCA ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini humo. Meja...
Published 05/20/24