Weka akiba mapema ikusaidie pale utakapo staafu
Listen now
Description
Maana akili zako zinakuwa zimebanwa kabisa unapata pesa na unazitumia kienyeji kienyeji tu. Ili uweze kuelewa tafuta watu waliostaafu. Wengi sana wana maisha mabaya na ni wachache sana wana maisha mazuri, kwa sababu wengine walikuwa na maisha mazuri sana walipokuwa kazini. Walikuwa na magari na nyumba kumbe ni za shirika au kampuni ambayo anafanyia kazi lakini sio vya kwake. Maana wakati wa zamani wafanyakazi walikuwa wanapewa kila kitu hadi furniture za ndani, ukiwaona utafikiri ni vya kwao kumbe sio vyao ni vya shirika akifukuzwa kazi au hiyo kazi ikiisha ndipo utaona namna maisha yake yanavyobadilika kabisa. Tulikuwa mkoa mmoja, tulikuta mchungaji ambaye alifariki ghafla akiwa kwenye safari ya kikazi. Aliacha watoto wake sita, mke wake na watoto wa ndugu zake sita. Kwa hiyo nyumbani kwake kulikuwa na watoto kumi na mbili. Mchungaji mpaka anakufa alikuwa hana nyumba. Baada ya mazishi na baada ya miezi mitatu kupita wazee wa kanisa na baadhi ya Viongozi wa lile kanisa wakimwendea yule mke wa mchungaji aliyefariki.Wakamuambia kuwa mama tunamshukuru Mungu kwa ajili yamume wako maana kwa kweli tuliona mkono wa Mungu juu yake sijui kwanini Mungu alimchukua mapema. Walianza mbali kuanza kuongea nae, na walisema mama unajua kilichotuleta ni kuwa mambo lazima yaende na Mungu katupatia mchungaji mwingine. Sasa tunahitaji hii nyumba ili aje aishi hapa. Yule mama alikuwa hana mahali pengine pa kwenda yule mama alitusimulia yeye mwenyewe maana anasema baada ya hapo alianza kulia na akapata pressure na akaugua muda mrefu sana. Ile kazi aliyokuwa anafanya alifukuzwa maana hakuonekana kazini muda mrefu sana kwa sababu ya kuumwa. Je unataka kwenda kiroho na future ya familia????, unakufa hujaacha mambo ya familia kikaa sawa, ukiondoka unawachia mama na watoto mzigo mzito sana.
More Episodes
Published 11/30/23
Published 07/26/21
Published 07/26/21