Mashirika ya UN yahaha kuwasaidia waathirika wa mizozo na ukame Baidoa Somalia
Listen now
Description
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO linasema idadi ya milipuko ya magonjwa iliyoripotiwa na pia dharura za kiafya zinazohusiana na tabianchi katika Ukanda wa Pembe ya Afrika zimefikia kiwango cha juu zaidi kuwahi kutokea karne hii, na hivyo kuzidisha janga la kiafya katika eneo ambalo watu milioni 47 tayari wanakabiliwa na njaa kali. Mfano wa hivi karibuni ni katika maeneo kadhaa ya Pembe ya Afrika kama Somalia. WHO na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa likiwemo la uhamiaji, IOM na wadau wengine wanashirikiana kuwasaidia watu waliko katika hatari zaidi kwenye maeneo mbalimbali ya somalia wakiwemo waliofurushwa katika maeneo ya viunga vya mji wa Baidoa. Makala hii iliyoandaliwa na WHO inasimuliwa kwa kina na Anold Kayanda.
More Episodes
Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII uliodumu kwa wiki mbili hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa umefikia tamati leo Aprili 26. Miongoni mwa masuala muhimu yaliyojadiliwa ni mabadiliko ya tabianchi na mazingira, likiwa ni suala ambalo pia miezi miwili...
Published 04/26/24
Huko nchini Sudan jimboni Darfur Kaskazini, hususan mjini El-Fasher na viunga vyake mapigano kati ya jeshi la serikali SAF na wanamgambo wa RSF yanazidi kuwa na madhara kwa rai ana kumtia hofu kubwa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk. Katika kufahamu hali iko vipi,...
Published 04/26/24