26 MACHI 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DR Congo ambako Umoja wa Mataifa unasema wananchi milioni 23.4 wanakabiliwa na njaa. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu SEA, machafuko DRC na vifo vya wahamiaji. Mashinani inamulika miradi ya maji nchini Tanzania.  Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Hatua Maalum za Ulinzi dhidi ya Unyonyaji na Unyanyasaji wa Kingono imewekwa wazi hii leo.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) limetoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka kutokana na ongezeko la hatari kwa watu waliokimbia makazi yao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Na wakati mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) unaohusu Wahamiaji Wasiofahamika waliko ukitimiza miaka kumi, ripoti mpya ya shirika hilo iliyopewa jina ‘Muongo mmoja wa kukusanya taarifa za vifo vya wahamiaji’ inaonesha mienendo ya kutisha ya vifo na kupotea kwa wahamiaji katika muongo mmoja uliopita na kwamba mtu mmoja kati ya watatu hufariki duniani katika harakati za kukimbia migogoro katika nchi yake.Katika mashinani tunakuletea ujumbe wa Mhandisi Denis Arbogast, Msimamizi wa mradi wa maji Kasulu mkoani Kigoma nchini Tanzania, mradi inayofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wake.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
More Episodes
Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa mwiba kwa jamii nyingi yakizilazimu kubadili mfumo wao wa Maisha ili kukabiliana na athari zake kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa jamii zilizoathirika na janga hilo ni za watu wa asili wakiwemo Wamaasai kutoka Kenya na hususan wanawake. Je wanahimili...
Published 05/01/24
Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za...
Published 05/01/24