Kituo cha malezi ya watoto nchini Kenya chatekeleza azma ya Umoja wa Mataifa
Listen now
Description
Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 ulifunga pazia hivi majuzi jijini New York Marekani ukipigia chepuo uwekezaji kwa wanawake na wasichana, na leo tunabisha hodi nchini Kenya wasichana waliokumbwa na ujauzito utotoni na kukatishwa ndoto za kuendelea na masomo au kupata ajira wamepata jawabu la changamoto wanazokumbana nazo pindi wakijifungua watoto wao. Changamoto kama vile mahali pa kumwacha mtoto kwa malezi ili aweze kuendelea na shule au kupata ajira.  Umoja wa Mataifa unasema kila mtu ana haki ya elimu hata kama amepata changamoto gani maishani. Na  ndipo ushirikiano kati ya mashirika ya kiraia lile la “Work for life”, pamoja na lile la “A Pack a Month”, linalohusika na utoaji wa misaada mbali mbali ikiwemo taulo za kike kwa wazazi wenye mahitaji na wasichana wanaokwenda shule walizindua kituo cha malezi ya watoto wachanga nyakati za mchana katika eneo la Ngong nchini Kenya. Mradi unaungwa mkono na wadau kadhaa ikiwemo serikali  ya Kenya. Selina Jerobon ni msimulizi wetu kupitia mada hii iliyofanikishwa na Redio washirika DOMUS ya huko Kenya. 
More Episodes
Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII uliodumu kwa wiki mbili hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa umefikia tamati leo Aprili 26. Miongoni mwa masuala muhimu yaliyojadiliwa ni mabadiliko ya tabianchi na mazingira, likiwa ni suala ambalo pia miezi miwili...
Published 04/26/24
Huko nchini Sudan jimboni Darfur Kaskazini, hususan mjini El-Fasher na viunga vyake mapigano kati ya jeshi la serikali SAF na wanamgambo wa RSF yanazidi kuwa na madhara kwa rai ana kumtia hofu kubwa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk. Katika kufahamu hali iko vipi,...
Published 04/26/24