Griffiths: Jaribio la kuitenga UNRWA lazima likome
Listen now
Description
Mratibu Mkuu wa Misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths amesema shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA ni uti wa mgongo wa operesheni za Kibinadamu Gaza hivyo jaribio la kulitenga shirika hilo lazima likome.  Bwana Griffiths ametoa kauli hiyo leo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X zamani Twitter akisistiza kuwa juhudi zozote za kusambaza misaada ya kibindamu kwenye Ukanda wa Gaza bila kupitia shirika la UNRWA haziwezi kufanikiwa na watu zaidi ya milioni 2 wanaitegemea UNRWA ili kuendelea kuishi.  Ameendelea kusema kwamba hadi sasa hakuna shirika lingine lolote lenye uwezo wa kufika kila kona ya Gaza, uzowefu na imani ya jamii ya kutekeleza majukumu yake kama lilivyo shirika la UNRWA. Wakati huohuo shirika la UNRWA limeonya kwamba mashambulizi ya Israel yameendelea tena usiku wa kuamkia leo huko Gaza Kaskazini Khan Younis na Rafah ambako watu milioni 1.2 wanapata hifadhi na kusababisha vifo zaidi. Huku lile la afya la Umoja wa Mataifa WHO likisema wakati timu yake ikiwa katika operesheni ya kibinadamu katika hospital ya Al-Aqsa jana Jumapili maeneo ya hospital yalipigwa na shambulio la anga lililokatili maiasha ya watu 4 na kujeruhi wengine 17. Nalo shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema linajitahidi kwa kila hali kutoa msaada wa chakula unaohitajika sana kwa watu milioni 1.45 Gaza lakini msaada huo hautoshi na bila usitishaji vita hawawezi kumfikia kila mtu na hivyo kufanya Maisha ya watu wengi kusalia hatarini.
More Episodes
Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa mwiba kwa jamii nyingi yakizilazimu kubadili mfumo wao wa Maisha ili kukabiliana na athari zake kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa jamii zilizoathirika na janga hilo ni za watu wa asili wakiwemo Wamaasai kutoka Kenya na hususan wanawake. Je wanahimili...
Published 05/01/24
Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za...
Published 05/01/24