Bado kazi ipo kupigania haki za mwanamke kote duniani - Paulina Ngurumwa
Listen now
Description
Kinara wa elimu nchini Tanzania Paulina Ngurumwa anasema bado kazi ipo kupigania haki za mwanamke kwa hiyo harakati hizo hazitakiwi kupoa. Paulina Ngurumwa ni mwanaharakati wa haki za kijamii kupitia shirika la KINNAPA Development Programme.  KINNAPA Development Programme ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa na wanajamii ya Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara, kaskazini mwa Tanzania likiwa ni chombo cha kutatua matatizo yao hasa ya ardhi. Shirika hili lilianzishwa mwaka 1992 na kwa miaka hiyo yote linajivunia kuendelea kufanikisha malengo yake na sasa hata limepanua mawanda ya huduma zake kama anavyoeleza mmoja wa viongozi Paulina Nguruma, katika mahojiano aliyoyafanya na Anold Kayanda wa Idhaa hii hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa. 
More Episodes
Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa mwiba kwa jamii nyingi yakizilazimu kubadili mfumo wao wa Maisha ili kukabiliana na athari zake kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa jamii zilizoathirika na janga hilo ni za watu wa asili wakiwemo Wamaasai kutoka Kenya na hususan wanawake. Je wanahimili...
Published 05/01/24
Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za...
Published 05/01/24