03 APRILI 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala inatupeleka nchini kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni? Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo kwa mara nyingine yameonya kwamba bila dalili zozote za usitishaji mapigano Gaza hali ya kibinadamu inaendelea kuwa janga huku mashambulizi ya Israel yakiendelea kukatili maisha, kufurusha watu na kusababisha uharibifu usioelezeka na njaa nayo ikiongeza hofu ya hatma ya watu wa eneo hilo.Siku zikizidi kuhesabiwa kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, kuondoka nchini humo, ujumbe huo unaendelea kutekeleza wajibu wake wa kujengea uwezo jeshi la serikali, FARDC kuweza kukabili vikundi vilivyojihami ambavyo vinatajwa kuhusika na asilimia 65 ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo mwezi Februari mwaka huu, kwa mujibu wa ripoti ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na serikali. Makala inatupeleka nchini kenya ambako serikali ya nchi hiyo kwa kushirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa wanaunda viashiria vipya ya kupima usawa wa kijinsia katika biashara.Na mashinani tunakupeleka nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu jinsi ambavyo miradi ya maji mkoani Kigoma inavyowasaidia wanfunzi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
More Episodes
Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa mwiba kwa jamii nyingi yakizilazimu kubadili mfumo wao wa Maisha ili kukabiliana na athari zake kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa jamii zilizoathirika na janga hilo ni za watu wa asili wakiwemo Wamaasai kutoka Kenya na hususan wanawake. Je wanahimili...
Published 05/01/24
Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za...
Published 05/01/24