05 APRILI 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunaangazia vita katika Ukanda wa Gaza ukielekea miezi siti hapo kesho, na programu ya mlo shuleni nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Rwanda na mashinani nchini DRC, kulikoni?”. Kesho kutwa jumapili ikiwa ndio itatimu miezi sita ya mzozo wa Gaza, huko Mashariki ya Kati, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo amezungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani akirejelea wito wake wa sitisho la mapigano kwa misinigi ya kiutu, kuachiliwa kwa mateka wote bila masharti, ulinzi wa raia na misaada ya kiutu ifikie walengwa bila vikwazo vyovyote huku akikgusia pia Israeli kutumia akili mnemba kwenye operesheni zake.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP nchini Sudan Kusini kupitia programu yake ya chakula shuleni imefanikiwa kuwasaidi wasichana wengi kuepukana na ndoa za utotoni. Katika makala Anold Kayanda anatupeleka nchini Rwanda kusikia programu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF Rwanda kudhibiti tatizo la changamoto ya afya ya akili kwa vijana balehe.Na katika mashinani tutaelekea nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC kusikia simulizi ya mkimbizi wa ndani”.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
More Episodes
Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa mwiba kwa jamii nyingi yakizilazimu kubadili mfumo wao wa Maisha ili kukabiliana na athari zake kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa jamii zilizoathirika na janga hilo ni za watu wa asili wakiwemo Wamaasai kutoka Kenya na hususan wanawake. Je wanahimili...
Published 05/01/24
Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za...
Published 05/01/24