08 APRILI 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunaangazia ombi la Palestina kujiunga rasmi kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa, na uwezeshaji wa wanake ambapo tunatembelea mkimbizi katika kambi ya Kakuma nchini Kenya. Makalatunakupeleka nchini DRC na mashinani nchini Tanzania. Huko Gaza, watoa misaada ya kibinadamu wakiwa na wasiwasi mkubwa juu ya mipango ya Israel kuvamia eneo la Rafah hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa Palestina imeanza mchakato wa kuwa mwanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa kwani hivi sasa ujumbe wake ni uangalizi usioipatia hadhi ya kupiga kura. Mchakato huo unaanzia ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Mwanamke akiwezeshwa anaweza, huo ndio umekuwa usemi wa Umoja wa Mataifa ukipigia chepuo wanawake kujumishwa katika kila Nyanja ya Maisha ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuchangia katika maendeleo ya jamii. Usemi huo unaungwa mkono na mwanamke mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambaye sasa anaishi Kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Katika makala makala ambapo Assumpta Massoi anatupeleka jimboni Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia manufaa ya uwepo wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO ambao sasa unafunga virago baada ya kuhudumu kwa miaka 22.Na katika mashinani tutakuwa Tanzania kuangalia endapo lengo la ujumuishwaji wanawake katika huduma za kifedha litatimia ifikapo mwaka 2030.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 
More Episodes
Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa mwiba kwa jamii nyingi yakizilazimu kubadili mfumo wao wa Maisha ili kukabiliana na athari zake kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa jamii zilizoathirika na janga hilo ni za watu wa asili wakiwemo Wamaasai kutoka Kenya na hususan wanawake. Je wanahimili...
Published 05/01/24
Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za...
Published 05/01/24