Mariam Suleiman: Wanawake tuna ujuzi, tuna uweo na tunaweza
Listen now
Description
Mwanamke akiwezeshwa anaweza, huo ndio umekuwa usemi wa Umoja wa Mataifa ukipigia chepuo wanawake kujumishwa katika kila Nyanja ya Maisha ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuchangia katika maendeleo ya jamii. Usemi huo unaungwa mkono na mwanamke mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambaye sasa anaishi Kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya.  Kutana na Mariam Suleiman ambaye kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR anasema vita ilimfungisha virago Congo DRC hadi hapa kambini Kakuma, ingawa ilimvurugia amani yake haikumkatishia ndoto zake za kuendelea na ufundi wa kuchomelea vyuma na pia kuwa mkufunzi wa kazi hiyo. “Katika kuchomelea vyuma ninafurahia sana kufanyakazi kazi hiyo ninapokwenda kazini na kujikuta ni mwanamke peke yangu uwanjani na hivyo ninajivunia sana kwa sababu sio kazi rahisi kwenda hapo ukiwa mwanamke peke yako katikati ya wanaume 15. Hivyo ninajivunia sana kuwa mchomelea vyuma na mkufunzi wa kuchomelea na kutengeneza vyuma” Kwa Mariam matunda ya kazi yake yako dhahiri. “Moja ya kazi zangu zinazovutia ambazo nimefanya ni lango kuu  la kliniki 4” Pamoja na mafanikio hayo Marian anatamani kusoma zaidi kuongeza ujuzi. “Nilisoma hadi daraja la sita hiyo ni ngazi ya Diploma. Natamani kuchimba ndani zaidi ya hii tasnia ya kuchomelea vyuma lakini hapa Kenya hatuna hiyo kozi. Ipo katika taasisi ya uchomeleaji vyuma ya Afrika Kusini. Ningependa kwenda huko na kusoma uchomeleaji vyuma chini ya maji.” Na kwa kuwa yeye ameweza anaamini hakuna kinachomshinda mwanamke kwani “Wanawake tuna uwezo, wanawake tuna ujuzi, wanawake tunaweza kufanyakazi zinazofanywa na wanaume, wanawake tunaweza kufurahia kazi zetu, wanawake hebu tusimame kidete tunaweza”
More Episodes
Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa mwiba kwa jamii nyingi yakizilazimu kubadili mfumo wao wa Maisha ili kukabiliana na athari zake kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa jamii zilizoathirika na janga hilo ni za watu wa asili wakiwemo Wamaasai kutoka Kenya na hususan wanawake. Je wanahimili...
Published 05/01/24
Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za...
Published 05/01/24