09 APRILI 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka mjini Kigali ambako kumbukumbu ya mauaji ya kimbari imefanyika mwishoni mwa wiki na itaendelea kwa siku 100. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani tunakupeleka nchini Sudan Kusini. Baada ya huduma ya ulinzi wa amani kwa zaidi ya miaka 20 huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, walinda amani kutoka China, hii leo wameondoka kutoka kambi yao iliyoko nje kidogo ya mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini, Bukavu ambako walishiriki kwa kiasi kikubwa katika ujenzi wa miundombinu.Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Olga Sarrado Mur katika mkutano na waandishi wa habari leo mjini Geneva, Uswisi ameeleza kwamba vita nchini Sudan ikikaribia kutimiza mwaka mmoja kamili na ikiendelea kupamba moto, idadi ya Wasudan waliolazimika kukimbia sasa imepita watu milioni 8.5, huku milioni 1.8 kati yao wakiwa wamevuka mipaka ya nchi. Na kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) iliyotolewa leo, idadi ya watu wanaofariki dunia kutokana na virusi vya homa ya ini inaongezeka. Ugonjwa huo ni wa pili kwa kusababisha vifo vya watu milioni 1.3 kwa mwaka, sawa na ugonjwa wa kifua kikuu, ambao ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababisha vifo vingi zaidi kwa sasa. Hata hivyo WHO inasema lengo la kutokomeza  Homa ya ini ifikapo 2030 bado linapaswa kufikiwa.Na katika mashinani tutaelekea nchini Sudan Kusini kusikia ujumbe kuhusu hatari vilipuzi na mabomu ya kutegwa ardhini, salia hapo tafadhali.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
More Episodes
Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa mwiba kwa jamii nyingi yakizilazimu kubadili mfumo wao wa Maisha ili kukabiliana na athari zake kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa jamii zilizoathirika na janga hilo ni za watu wa asili wakiwemo Wamaasai kutoka Kenya na hususan wanawake. Je wanahimili...
Published 05/01/24
Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za...
Published 05/01/24