12 APRILI 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunaangazia kumbukizi wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, na wakimbizi wa Sudan wanaovuka mpaka kuelekea nchini Sudan Kusini. Makala na mashinani tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni? Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Baraza Kuu limekuwa na tukio maalum la kumbukizi ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda au KWIBUKA30, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo, Antonio Guterres ametumia hotuba yake pamoja na mambo mengine kuwasihi vijana kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki kukemea chuki kokote wanapoisikia au kuiona.Tarehe 15 April wiki ijayo siku ya jumatatu nchi ya Sudan itatimiza mwaka mmoja rasmi tangu kuanza kwa mzozo kati ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na Vikosi vya jeshi la Sudan (SAF). Vita hiyo imesababisha maelfu ya watu kuwa wakimbizi wa ndani na wengine kusaka hifadhi nchi Jirani. Mashirika ya misaada ya kibinadamu nayo yamekuwa mstari wa mbele kusaidia wananchi wenye uhitaji japo yanakabiliwa na ufinyu wa bajeti. Makala tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako kikosi cha 11 cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT-11 kinachohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO wametekeleza wajibu wao wa kulinda raia kwa kuwapatia huduma ya matibabu kwenye Kijiji cha Matembo kilichoko mjini Beni jimboni Kivu Kaskazini.Na mashinani tunakuletea ujumbe wa Marthe Nyangoma, mtumishi wa umma kutoka eneo la Irumu, huko Ituri nchini DRC, ambaye kwa uwezeshaji wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa MONUSCO, anahamasisha jamii dhidi ya taarifa potofu na kauli za chuki akisistiza kuwa kabla ya kuwasilisha taarifa, lazima zidhibitishwe ili kuepusha mgawanyiko.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
More Episodes
Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa mwiba kwa jamii nyingi yakizilazimu kubadili mfumo wao wa Maisha ili kukabiliana na athari zake kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa jamii zilizoathirika na janga hilo ni za watu wa asili wakiwemo Wamaasai kutoka Kenya na hususan wanawake. Je wanahimili...
Published 05/01/24
Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za...
Published 05/01/24