Jukwaa la Jamii za watu wa asili lafungua pazia katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa
Listen now
Description
Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa jijini New York Marekani, Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili limeanza rasmi na litadumu kwa muda wa wiki mbili likiwaleta pamoja zaidi ya washiriki 2000 wa jamii za asili kutoka kila pembe ya dunia kujadili masuala mbalimbali.  Hiki ni kikao cha 23 cha jukwaa hili la kudumu la watu wa jamii za asili ambao leo mkutano wa kwanza umefunguliwa rasmi ukihudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa akiwemo Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Balozi Dennis Francis.  Majadiliano ya wiki mbili za mkutano huu yataongozwa na dhima ya kuangazia haki za watu wa asili kujitawala pamoja na sauti za vijana wa jamii ya asili.  Sehemu muhimu ya majadiliano haya inalenga kuhakikisha watu wa jamii za asili wanapata haki ya kujiamulia na kupata ufadhili utakao wawezesha kudai haki zao vyema, kuendeleza maendeleo yao ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni na kufadhili miundo ya utawala wao, kama ilivyoainishwa katika Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Watu wa Kiasili. Mwenyekiti wa Jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusuu watu wa asili Bi. Hindou Oumarou Ibrahim akizungumza katika jukwaa hilo amesema “Kuondolewa vikwazo kwenye upatikanaji wa fedha ni muhimu ili kuhakikisha watu wa asili wanatekeleza kwa vitendo mipango yao na kuwa na njia ya kudumisha kujitawala,”  Kwa upande wake Bwana Li Junhua, ambaye ni msaidizi waKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kiuchumi na kijamii (DESA) amesema “unahitaji ufadhili wa muda mrefu, unaotabirika, na wa moja kwa moja kwa Watu wa Asili, ikijumuisha kupitia mifumo ya ufadhili ya umma, ya kibinafsi, na inayoongozwa na Wenyeji ambayo inashirikisha kikamilifu Wanawake na vijana wa kiasili.” Unaweza kufuatilia moja kwa moja matangazo ya jukwaa hili yanayorushwa mubashara na Umoja wa Mataifa kupitia wavuti wake wa UN Web TV,matangazo yanarushwa kwa lugha rasmi sita za umoja wa Mataifa ambazo ni Kingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kichina, Kispanishi na Kirusi.
More Episodes
Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa mwiba kwa jamii nyingi yakizilazimu kubadili mfumo wao wa Maisha ili kukabiliana na athari zake kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa jamii zilizoathirika na janga hilo ni za watu wa asili wakiwemo Wamaasai kutoka Kenya na hususan wanawake. Je wanahimili...
Published 05/01/24
Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za...
Published 05/01/24