UNICEF: Miaka 10 ya watoto kutekwa Chibok, bado hakuna mifumo ya ulinzi
Listen now
Description
Nigeria inapotimiza miaka 10 tangu tukio la utekwaji nyara la watoto wa kike 275 huko Chibok, kaskazini magharibi mwa taifa hilo, hadi sasa bado watoto 90 wamesalia mateka na nchi hiyo inasalia na kumbukumbu ya tukio linguine la wanafunzi wa shule kutekwa nyara jimboni Kaduna mwezi Machi mwaka huu, hali inayosababisha Umoja wa Mataifa kutoa wito mahsusi.   Ilikuwa usiku wa tarehe 15, Jumatatu ndipo watoto hao wa kike wenye umri wa kati ya miaka 12 hadi 17 walitekwa na kundi la Boko Haram huko jimboni Borno, na ndio maana kwa mazingira yalivyo sasa, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema safari bado ni ndefu kwa watoto nchini Nigeria kutimiza ndoto yao ya kusoma kwenye mazingira yaliyo salama, kwani ni asilimia 37 tu ya shule kwenye majimbo 10 yaliyo kwenye mazingira hatarishi ndio zina mifumo ya kubaini mapema vitisho kama vile shule kushambuliwa.  Ripoti ya UNICEF iliyotolewa leo Abuja, miji Mkuu wa Nigeira ikipatiwa jina Viwango vya Chini Vya Usalama Shuleni au MSSS kwa lugha ya kiingereza, inaonesha ukweli mchungu wa kufanikisha safari hiyo kwa mtoto nchini Nigeria kuweko shuleni bila uoga.  Mwakilishi wa UNICEF nchini humo Cristian Munduate amesema tukio la kutekwa nyara wasichana wa Chibok ni kengela ya kutuamsha juu ya hatari kubwa watoto wetu wanakabiliwa nayo wanaposaka elimu.  Anasema leo tunapotafakari janga hili na mengine ya hivi karibuni ni dhahiri kuwa juhudi zetu za kulinda mustakabali wa watoto wetu lazima ziimarishwe.  Mwakilishi huyo anasema kwa kuzingatia takwimu zilizotolewa na ambazo zinatia hofu kubwa, ni lazima kupata majawabu ya sio tu dalili bali pia chanzo cha janga hilo la utekaji nyara watoto.  Bi. Munduate amekumbusha kuwa elimu ni haki ya msingi na ni njia muhimu ya kuelekea kuondokana na umaskini. Lakini kwa watoto wengi nchini Nigeria inasalia kuwa ndoto isiyotimizika.  Ripoti ilimulika maeneo 6 ikiwemo mifumo thabiti ya shule, ukatili dhidi ya watoto, majanga ya asili,mizozo ya kila siku na miunmdombinu ya shule na kubaini utofauti mkubwa wa vigezo hivyo katika majimbo yote 36.  Jimbo la Borno liko thabiti kwani limekidhi viwango kwa asilimia 70 ilhali majimbo ya Kaduna na Sokoto bado yako nyuma.  Uchambuzi huu unakuja wakati kuna ripoti za ongezeko la ghasia dhidi ya shule ambapo katika miaka 10 iliyopita, matukio ya mashambulizi yamesababisha watoto zaidi ya 1,680 kutekwa nyara wakiwa shuleni au kwinigneko.  UNICEF inataka Nigeria pamoja na mambo mengine ihakikishe shule kwenye majimbo yote zina rasilimali za kutekeleza MSSS.  Pia itatue pengo la uwiano wa usawa katika hatua za kuimarisha usalama shuleni. Nigeria pia iimarishe usimamizi wa sheria na mikakati ya usalama ya kulinda taasisi za elimu na jamii dhidi ya utekwaji.  Kwa sasa UNICEF inashirikiana na serikali kuhakikisha kila mtoto anakuwa na mazingira salama ya kusomea.  Soma ripoti nzima hapa.
More Episodes
Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa mwiba kwa jamii nyingi yakizilazimu kubadili mfumo wao wa Maisha ili kukabiliana na athari zake kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa jamii zilizoathirika na janga hilo ni za watu wa asili wakiwemo Wamaasai kutoka Kenya na hususan wanawake. Je wanahimili...
Published 05/01/24
Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za...
Published 05/01/24