16 APRILI 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Tanzania, Abeida Rashid Abdallah anafafanua kwa nini Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Zanzibar ni chanda na pete.  Pia tunakuletea muhtasari ya habari na mashinani kama zifuatazo. Leo mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kuonya juu ya vita inayoendelea kukatili maisha ya watu Gaza, na kusambaratisha miundombinu yakitaja kuwa wanawake karibu 10,000 wamepoteza Maisha tangu vita kuanza miezi sita iliyopita huku mtoto mmoja anajeruhiwa au kuuawa kila dakika 10.Jukwaa la vijana la Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC leo limeng’oa nanga hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Matrekani likiwaleta maelfu ya vijana kutoka kila kona ya Dunia. Joramu Nkumbi ni miongoni mwa washiriki wa jukwaa hilo kutoka Tanzania na anafafanua wanachokijadili mwaka huu.  Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM kwa shirikiana na mashirika mengine 48 ya kibinadamu, ya maendeleo na serikali wametoa ombi la haraka la dola milioni 112 ili kuwasaidia zaidi ya wahamiaji milioni 2.1 na jamii zinazowahifadhi. Kwa mujibu wa IOM wahamiaji na jamii hizo ni katika njia za uhamiaji za Mashariki na Kusini zkijumuisha Djibouti, Ethiopia, Somalia, Yemen, Kenya na Tanzania.Na mashinani leo tunakwenda mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC hususan jimboni Ituri ambako huko ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO umechukua hatua kukabili mashambulizi kutoka waasi, mashambulizi ambayo kila uchao yanazidi kufurusha raia. Mzungumzaji wetu ni Luteni Kanali Mensah Kedagni, msemaji wa kijeshi wa MONUSCO.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
More Episodes
Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII limekunja jamvi mwishoni mwa wiki hapa Umoja wa Mataifa baada ya wiki mbiliza kujadili masuala mbalimbali  ikiwemo mchango wa jamii hizo katika kudumisha amani Adam Kulet Ole Mwarabu Ole Mareka kutoka jamii ya Wamaasai wa...
Published 04/30/24
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, Adam Kulet Ole Mwarabu Ole Mareka kutoka jamii ya Wamaasai wa Parakuyo iliyoko mjini Morogoro nchini Tanzania anazungumza na Flora Nducha. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani. Kamishina Mkuu wa sririka la Umoja wa Mataifa la msaada kwa...
Published 04/30/24