Dkt. Moeti: Shukrani kwa kila mmoja achangiaye damu Afrika
Listen now
Description
Ikiwa leo ni siku ya uchangiaji damu duniani, Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO, Kanda ya Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti ametoa shukrani kwa kila mtu anayejitoa kuchangia damu barani Afrika, akisema kila mchango wa damu ni nguzo ya matumaini kwa uhai wa binadamu mwingine aliye kwenye uhitaji lakini hasama zaidi inahitajika. Amesema Dkt. Matshidiso Moeti, Mkurugenzi huyu wa WHO kanda ya Afrika katika ukurasa wake wa X, kwenye ujumbe wake wa siku ya leo ya uchangiaji damu duniani, maudhui yakiwa Miaka 20 ya kuchangia: Asanteni Wachangiaji wa damu. Anashukuru wachangiaji wote wa damu barani Afrika. Akisema wanaokoa maisha. Na zaidi ya yote anapenda kuwahamasisha wawe wachangiaji wa damu mara kwa mara. “Nimekutana na mabingwa kadhaa ambao wamekuwa wakichangia damu kwa muongo mmoja au zaidi. Hili ni jambo ambalo tunafanya mara moja kwa mwaka pindi tunaposherehekea siku hii kama leo, lakini kwa kawaida mara tatu au mara nne kwa mwaka.” Lakini ni nini kinahitajika? “Tunahitaji kuhamasisha watu kujitolea zaidi kuchangia damu barani Afrika. Hali inazidi kuimarika lakini bado safari ni ndefu.” Kulikoni safari ni ndefu? Kwa sababu tunahitaji kuongeza maradufu uchangiaji wa damu angalau Afrika. Kwa sasa kiwango chetu ni Uniti 5 za damu kwa watu 100. Tunahitaji angalau uniti 10 kwa watu 1000. Kwa hiyo jitokezeni mara kwa mara.” Akaelekeza wito kwa kundi mahsusi.. “Njooni kila mwaka. Hebu tuwahusishe vijana na tuweze kuimarisha hali ya afya kwa wakazi wa Afrika.” WHO inasema damu salama inaokoa maisha na uchangiaji wa damu mara kwa mara kutoka kwa watu wenye afya kunahitajika ili kuhakikisha damu inapatikana wakati wowote pale inapohitajika. 
More Episodes
Nchini Tanzania, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) linaendesha programu ya mafunzo yanayolenga kuboresha ujuzi wa wataalamu wa mifugo katika kudhibiti magonjwa ya wanyama na kuimarisha afya ya mifugo ili kuihakikishia jamii uhakika wa chakula na chakula salama. John Kabambala...
Published 06/25/24
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulikaza juhudi za  kuimarisha afya ya mifugo ili kuihakikishia jamii uhakika wa chakula na chakula salama. Pia tunakuletea muhutasari wa habari zikiwemo za Gaza, mabaharia, na ripoti ya ya matumizi ya pombe. Mashinani...
Published 06/25/24