25 JUNI 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulikaza juhudi za  kuimarisha afya ya mifugo ili kuihakikishia jamii uhakika wa chakula na chakula salama. Pia tunakuletea muhutasari wa habari zikiwemo za Gaza, mabaharia, na ripoti ya ya matumizi ya pombe. Mashinani tunasalia na siku ya mabaharia duniani.  Katika Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati tathmini mpya iliyofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula Duniani WFP imethibitisha wasiwasi wa kuendelea kuwepo kwa viwango vya njaa ambapo asilimia 96 ya wananchi wanakabiliwa na uhaba wa chakula.Leo ni siku ya mabaharia duniani ikibeba maudhui ya kuangalia usalama wao kazini. Katika ujumbe wake kwa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka kukomeshwa kwa vitendo vya kiharamia vya meli kutekwa nyara na kueleza kuwa mabaharia hawapaswi kuwa waathiriwa wa migogoro ya kijiografia na kisiasa.Na ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO imeonesha vifo milioni 2.6 kwa mwaka vinachangiwa na unywaji pombe hii ikiwa ni sawa na asilimia 4.7 ya vifo vyote duniani, na vifo laki sita kwa matumizi ya dawa za kulevya.Mashinani leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya mabaharia, na kupitia ujumbe wake wa siku hii Katibu Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya baharí, IMO Arsenio Dominguez anawatakia kila la heri mabaharia wote akiwaalika katika meza ya kubonga bongo kuhusu masuala ya usalama wa baharini.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
More Episodes
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Chombo cha kuzama hakina usukani.”
Published 06/27/24
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ikiangaazia hafla maalum ya UNICEF na wadau wake pamoja na wasanii iliyofanyika Nairobi Kenya, mada ikiwa “Ungana na watoto wa Sudan”. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za maandamano Kenya, Janga la njaa Sudan, na MSMEs. Katika kujifunza...
Published 06/27/24