27 JUNI 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ikiangaazia hafla maalum ya UNICEF na wadau wake pamoja na wasanii iliyofanyika Nairobi Kenya, mada ikiwa “Ungana na watoto wa Sudan”. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za maandamano Kenya, Janga la njaa Sudan, na MSMEs. Katika kujifunza kiswahili tunakuletea uchambuzi wa methali. Kufuatia madhila yaliyotokana na maandamano makubwa nchini Kenya dhidi ya mswada wa fedha, leo Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR imeeleza kwamba Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk amesikitishwa na vifo na kujeruhiwa kwa watu.Zaidi ya Wasudan milioni 25 yaani zaidi ya nusu ya idadi ya watu wote nchini humo wanakabiliwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa ya viwango vya Uhakika wa Chakula (IPC) kutokana na tathimini iliyofanywa kati ya mwishoni mwa mwezi Aprili na mapema mwezi huu wa Juni.Na ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya biashara ndogo sana, ndogo na za ukubwa wa kati, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku hii amesisitiza jukumu muhimu la wajasiriamali hao katika uchumi wa kimataifa, ikiangaziwa michango yao katika uundaji wa nafasi za kazi, ukuaji wa uchumi, na uwezeshaji wa makundi mbalimbali yaliyotengwa.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Chombo cha kuzama hakina usukani.”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
More Episodes
Makala hii inatupeleka nchini Tanzania ambapo Assumpta Massoi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Tanzania anamulika usaidizi wa shirika hilo kwa manusura wa mafuriko yaliyokumba taifa hilo la Afrika Mashariki. 
Published 06/28/24
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya mwaka 2024 ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs, na juhudi za mashirika ya Umoja wa Mataifa za kuwawezesha wakulima nchini Somalia. Makala tunakupeleka nchini Tanzania, na mashinani ujumbe ubunifu na vijana barani Afrika. Bila uwekezaji mkubwa na kuongeza...
Published 06/28/24