28 JUNI 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya mwaka 2024 ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs, na juhudi za mashirika ya Umoja wa Mataifa za kuwawezesha wakulima nchini Somalia. Makala tunakupeleka nchini Tanzania, na mashinani ujumbe ubunifu na vijana barani Afrika. Bila uwekezaji mkubwa na kuongeza hatua, kufikiwa kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs kutasalia kuwa mgumu, imeonya Ripoti ya mwaka huu 2024 kuhusu mwenendo wa utekelezaji wa malengo hayo ikiwa imesalia miaka sita pekee kufikia muda ambao ulimwengu ulijiwekea kuwa umeyatimiza malengo yote 17.Huku takriban watu milioni 7 nchini Somalia wakihitaji msaada wa kuokoa maisha mwaka huu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO linahimiza jumuiya ya kimataifa kuendelea kuunga mkono Wasomali wanaokabiliwa na athari za njaa,mabadiliko ya tabianchi, migogoro na kufurushwa makwao.Katika makala Assumpta Massoi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Tanzania anamulika usaidizi wa shirika hilo kwa manusura wa mafuriko yaliyokumba taifa hilo la Afrika Mashariki.Mashinani tutasikia jinsi shirika la umoja wa mataifa la Afya ulimwenguni, WHO linakuza ubunifu miongoni mwa wanasayansi vijana wa afya barani Afrika      ili kuboresha ufanisi, ubora wa huduma za afya  na maendeleo katika matibabu na tiba.”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
More Episodes
Hii leo jaridani tunaangazia tukio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Julai Mosi la kuidhinisha tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani kama zifutazo… Huko Gaza shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia...
Published 07/02/24
Kutokana na hali tete ya usalama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Umoja wa Mataifa kwa miaka mingi umekuwa ukifanya juhudi za kuleta amani na kuilinda kwa kutuma ujumbe wake, MINUSCA ambapo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa huchangia vikosi mbalimbali. Kikosi cha 7 kutoka Tanzania, TANBAT 7 ni...
Published 07/01/24