02 JULAI 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunaangazia tukio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Julai Mosi la kuidhinisha tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani kama zifutazo… Huko Gaza shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA linasema wiki chache tu baada ya jeshi la Israeli kulazimisha watu kurejea mji wa Khan Younis ulioharibiwa, leo hii mamlaka za Israeli zimetoa amri mpya ya kuhama kutoka eneo hilo licha ya kwamba hakuna pahala paliko salama Ukanda wa Gaza. Watu 250,000 watalazimika kuhama tena.Nchini Sudan vita ikiendelea kurindima, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeziongeza Libya na Uganda kama nchi zinazopokea wakimbizi kutoka Sudan na hivyo kufanya nchi zinazowapokea kufikia saba zikiwemo Libya, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini, Chad na Ethiopia, na sasa linahitaji fedha dola bilioni 1.5 badala ya dola bilioni 1.4 iliyotangazwa awali.Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Bruno Lemarquis, amelaani vikali shambulio la tarehe 30 Juni mwaka huu dhidi ya msafara wa shehena za misaada ya kiutu huko Butembo jimboni Kivu Kaskazini, shambulio lililosababisha vifo vya wahudumu wawili wa misaada ya kibinadamu. Bwana Lemarquis ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki za watumishi hao.Na katika mashinani tutamsikia Estelle Zadra wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na utamaduni (UNESCO) akieleza mikakati yao katika kukuza lugha ya Kiswahili duniani.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
More Episodes
Hii leo jaridani tunaangazia tunaangazia maadhimisho ya tatu ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani maudhui yakiwa nafasi ya elimu ya sanaa. Makala tunatupeleka nchini Ghana kumulika umahiri wa wanafunzi wa Kiswahili, na mashinani tunakupeleka nchini China kusikia ujumbe wa mdau kuhusu lugha y...
Published 07/03/24
Hii leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika maadhimisho ya tatu ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani maudhui yakiwa nafasi ya elimu ya sanaa katika kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili. Maadhimisho haya yanafanyika tarehe 3 kwa kuwa siku yenyewe ya Kiswahili duniani yaani tarehe...
Published 07/03/24