Hizi ndizo shughuli zetu CIMIC ya TANBAT 7 - Kapteni John Zablon Mashamy
Listen now
Description
Kutokana na hali tete ya usalama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Umoja wa Mataifa kwa miaka mingi umekuwa ukifanya juhudi za kuleta amani na kuilinda kwa kutuma ujumbe wake, MINUSCA ambapo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa huchangia vikosi mbalimbali. Kikosi cha 7 kutoka Tanzania, TANBAT 7 ni miongoni mwa walinda amani waliko huko, hususani wakihudumu katika eneo la Berbérati, magharibi mwa nchi. Kupitia makala hii, Afisa uhusiano wa TABAT 7, Kapteni John Zablon Mshamy anaeleza shughuli zinazofanywa na kitengo cha uhusiano, CIMIC anachokiongoza.
More Episodes
Hii leo jaridani tunaangazia tunaangazia maadhimisho ya tatu ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani maudhui yakiwa nafasi ya elimu ya sanaa. Makala tunatupeleka nchini Ghana kumulika umahiri wa wanafunzi wa Kiswahili, na mashinani tunakupeleka nchini China kusikia ujumbe wa mdau kuhusu lugha y...
Published 07/03/24
Hii leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika maadhimisho ya tatu ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani maudhui yakiwa nafasi ya elimu ya sanaa katika kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili. Maadhimisho haya yanafanyika tarehe 3 kwa kuwa siku yenyewe ya Kiswahili duniani yaani tarehe...
Published 07/03/24