Only Way Up
Listen now
Description
Kutana Babuu wa Kitaa, Super Star, mkali kutoka King’oko, mwana hiphop, na mtangazaji kutoka moja kati ya vyombo vikubwa sana vya habari hapa nchini Tanzania. Kwa macho ya nje, Babuu ni kijana anayeishi ndoto za watu wengi sana. Kijana, maarufu, ana kazi nzuri, ana familią changa. Nadhani hii ni ndoto ya kila mwanaume. Lakini, kitu ambacho wengi tulikuwa hatukitambui, ni kwamba Babuu anapambana na vita kali sana ndani ya mwili wake na kwenye maisha yake binafsi. Maisha ya Babuu wa kitaa yalibadilika mara baada ya kugundulika kwamba ana saratanı ya ngozi, lakini pia mmoja kati ya watoto zake watatu anasumbuliwa na “Down syndrome” Pamoja na yote hayo, Babuu hajakubali changamoto hizi zimrudishe nyuma na kumfanya kuishi kinyonge. Ameendelea kuwa Babuu yule yule ambae wengi tunamfahamu, na kwa sasa anasisitiza kuwa kubali changamoto zako, na njia pekee ya kupambana nazo ni kwa kuangalia na kusonga mbele na juu . “ONLY WAY UP” Anaketi na Michael pamoja na Nadia, kwa pamoja wanazungumzia vita ya Babuu dhidi ya saratani aliyokutwa nayo, maisha yake kama baba anaelea mtoto ambae yupo tofauti na watoto wengine, na ni vipi ameweza kubaki kuwa Babuu yule yule ambae wote tunamfahamu kati kati ya changamoto zote hizi anazopitia? Na kwanini anaamini sana katika slogan yake ya “ONLY WAY UP”? Subscribe kwenye channel yetu ya YouTube, utazame na kusikiliza mazungumzo haya ya kusisimua na yenye mafunzo mengi sana kuhusu maisha. 
More Episodes
Get ready for an unfiltered, dynamic conversation about relationships from a man's perspective! Join us as a group of brothers come together to share raw insights, powerful truths, and fresh perspectives on how men can navigate modern relationships and be their best selves. In today's...
Published 04/23/24
Published 04/23/24
This is the Allan Lucky’s story of how he went against all odds to become the man he is today. Born in Songea, to a christian Family, Allan describes his early life as being constrained in the triangle of three main things, church, school and home. From an early age it seemed that this is how...
Published 04/02/24