Men and Healing
Listen now
Description
Katika “episode” yetu ya leo, wanaume wawili wameketi na kuulizana, kweli kuna mwanaume aliyepona? “A healed man”?  Tunaposema “A healed man” au mwanaume aliyepona, hapa tuna maanisha mwanaume ambaye amechukua muda wake kujitambua na kujua mapungufu yake, historia yake, sababu ya kwanini yupo jinsi alivyo, amejifunza kutokana na makosa yake, na pia yupo katika mapambano ya kumfanya awe mwanaume bora zaidi siku za usoni.   Kwa mujibu wa mgeni wetu wa leo, ndugu Leslie Omwenga, anasema hakuna kitu kama hicho. Hakuna kitu kama “A healed man”, na sababu kuu ya yeye kusema hivyo ni kwamba anaamini kila mwanaume ana kazi ya kuendelea kupambania afya yake ya akili mpaka siku ya mwisho, hivyo kwake kuna “A healing man”. Au mwanaume anayepona.  Huyu ni mwanaume ambaye kila siku anataka kuendelea kuwa bora, na anatakiwa afanye hivi mpaka siku ya mwisho ya uhai wake.   Leslie pamoja na Michael Baruti wanajadili swala hili kiundani, huku kila mmoja akichangia kwenye hili kutokana na uzoefu wake pamoja na ufahamu wake kuhusu mchakato mzima wa kumfanya mwanaume kuwa bora. Hakuna kitu ambacho hakikuguswa hapa, kuanzia malezi, mahusiano, swala zima la kipato, pamoja na swala zima la kumpeleka mwenzi wako ukweni kwake 😂😂.   Karibu katika episode ya leo.
More Episodes
Get ready for an unfiltered, dynamic conversation about relationships from a man's perspective! Join us as a group of brothers come together to share raw insights, powerful truths, and fresh perspectives on how men can navigate modern relationships and be their best selves. In today's...
Published 04/23/24
Published 04/23/24
This is the Allan Lucky’s story of how he went against all odds to become the man he is today. Born in Songea, to a christian Family, Allan describes his early life as being constrained in the triangle of three main things, church, school and home. From an early age it seemed that this is how...
Published 04/02/24