Episodes
Umoja wa Mataifa umeanza kuwaondowa wafanyakazi wake wasio na majukumu muhimu nchini Haiti kutokana na kuongezeka kwa ghasia na ukosefu wa usalama katika taifa hilo la Caribean.
Published 03/15/24
Baraza la Wawakilishi la Marekani, Jumatano liliidhinisha mswada, wa kuilazimisha programu maarufu ya mtandao wa kijamii, TikTok, kujitenga na kampuni mama, inayomilikiwa na China, ya ByteDance au kuuza sehemu ya programu hiyo kwa Marekani.
Published 03/14/24
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Published 03/13/24
Afisi ya Wizara ya Fedha ya  Marekani inayohusika na Udhibiti wa Mali za Kigeni (OFAC), Jumatatu imeyawekea vikwazo mashirika 16 na watu binafsi, ambao inasema wanahusika katika mtandao mpana wa biashara unaozunguka Pembe ya Afrika, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Cyprus.
Published 03/12/24
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Published 03/11/24
Ali Hassan Mwinyi, ambaye katika awamu mbili kama rais wa Tanzania alisimamia kuanzishwa kwa demokrasia ya vyama vingi na kuanzishwa kwa uchumi huria, amefariki akiwa na umri wa miaka 98.
Published 03/01/24
Marekani Jumatano ilisema "imefadhaishwa mno" na kupitishwa kwa mswada wa sheria kali dhidi ya wapenzi wa jinsia moja, na bunge la Ghana, na kuhimiza utathminiwe upya, ili kubaini kama unafuata katiba ya nchi hiyo.
Published 02/29/24
Watu 31 walifariki nchini Mali Jumanne na wengine 10 kujeruhiwa wakati basi lililokuwa linasafiri kuelekea Burkina Faso lilipoanguka kutoka kwenye daraja kusini mashariki mwa nchi hiyo, wizara ya uchukuzi ilisema.
Published 02/28/24
Sweden inatarajiwa kujiunga rasmi na NATO katika siku au wiki zijazo, baada ya Hungary hatimaye kutoa idhini yake siku ya Jumatatu – mwanachama wa mwisho kufanya hivyo.
Published 02/27/24
Jumuiya ya kiuchumi ya Ukanda wa Afrika Magharibi, ECOWAS, Jumamosi iliondoa baadhi ya vikwazo ilivyokuwa imeiwekea Nige,r baada ya mapinduzi ya kijeshi ya mwaka jana, yaliyomuondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum.
Published 02/26/24
Wagombea 15 kwenye uchaguzi ulioahirishwa nchini Senegal wamemshtumu Rais Macky Sall kuwa na nia mbaya na wameapa kuchukua hatua kuhakikisha tarehe mpya ya uchaguzi inatangazwa kwa haraka.
Published 02/22/24