Episodes
Usawa wa kijinsia katika mataifa mengi hapa Africa ni swala ambalo limekuwa kama donda sugu kwa kina mama, hali ambayo imefanya baadhi kujitoa, kuhakikisha kuwa swala hili linashugulikiwa na viongozi walio madarkani.   Skiza makala haya kwa ufahamu mengi
Published 11/23/21
  Pamekuwa na kempeni ya kumaliza bidhaa ya Tobacco katika matifa mengi ya Africa, kutokana na athari ya bidhaa hizo kwa afya ya bindamu, lakini wahusika katika sekta inayopinga matumizi ya wanalalamikia ugumu wa serikali katika kutekeleza sheria za kupinga matumizi ya bidhaa hizi. Skiza makala haya kwa  mengi zaidi.
Published 10/18/21
Rais wa Uganda amependekeza dhamana ya kuondolewa kwenye kifungu cha katiba ya taifa hilo, akidai inatumika visivyo. Makala haya yanaangazia athari ya kuondelewa kwa kifungo hicho kwa katiba ya Uganda.
Published 10/18/21
Luhga ya ishara ni moja ya lugha ambazo zimeanza kutiliwa maanani na mataifa mbalimbali kwa manufaa ya kuwasiliana bila vikwazo na ndugu na dada zetu ambao wanaishi na ulemavu kuskia. Kwa mengi zaidi skiza makala haya.
Published 10/06/21
Shirika la kutetea haki za binadamu ya Human Right Watch, limetuhumu serikali ya Kenya, kwa kukosa walinda kina dada dhidi ya dhuluma za kijinsia.
Published 09/27/21
Familia nyingi za mashambulizi yanayotokana na wanajihadi, zinaendelea kudai fidia huku zikituhumu serikali zao kwa kukosa kuhakikisha wanapata haki.
Published 09/27/21
katika makala haya tunatofautisha haki za raia na usalama wao, kumekuwa na mjadala kuhusu raia kulalamika wakidai kuwa maafisa wa usalama wamekuwa wakivuka mipaka wakati wakapokabiliana na washukiwa. Mtaalamu wa usalama Tuta Richard, anatoa ufafanuzi kwenye makala haya.
Published 09/06/21
Kwenye makala haya tunajikita kwenye haki za wanawake kuwania au kuteuliwa kwenye nyadhifa mbalimbali za uongozi katika bara la Africa hasa Africa Mashariki. Mwenyekiti wa chama cha mawili wanawake nchini Kenya, FIDA, Nacy Ikinu, Mbunge Milly Odhiambo kutoka Kenya,  na Lucy Githaika ambaye ni mkurungezi wa shirika la kutetea wanawake la Diakonia, wanashiriki mahakala haya.
Published 08/31/21
Katika makala haya Benson wakoli anazungumza  na wakili Ojwang Agina, anayetoa mtazamo wa kisheria kuhusu  haki za raia wanaokimbia Afghanistan na mwanahistoria , Lugete Mussa Lugete,  ataeleza ni vipi taifa la Afghanistan limejipata kwenye nafasi ya sasa.
Published 08/23/21
Katika makala haya  tunaangazia haki za mnyama punda  ambaye ametejwa kuwa muhimu sana katika sekta ya uchukuzi na hata kuimarisha uchumi kwa kuwapa ajira raia wanaowafuga.
Published 08/16/21
Wiki hii tunaangazia haki za wananchi kutoka mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na tunathathmini Jumuiya hiyo kwa kina.
Published 08/02/21
Visa vya uvamizi au vita vya kikabila vimechangia sana, watoto kupoteleana na familia zao, baadhi ya mashariki yakilazimika kuchukua hatua ya kupatanisha watoto waliopotea na familia zao. katika makala haya bado Benson wakoli anazungumza na Jeffa Jenga Mbungwa, mkurugezi mkuu wa shirika la Grass root Epowerement and development organization, linaloendesha shughuli zake nchini Sudan Kusini
Published 07/26/21
Taifa la Sudan Kusini limeshutumiwa na umoja wa mataifa kwa kukiuka haki mbalimbali za binadamu moja wepo ikiwa kuwasajili watoto kuwa wanajeshi. Katika makala haya  Jeffa mbugwa Njenga,  ni mkurugezi mkuu wa shirika lisilokuwa la kiserekali la Grass Root empowerement and deveopment organization, ambalo linajishuhulisha na shughuli mbali mbali za kusaidia  raia sudan Kusini, kuu likiwa kuwasadia watoto ambao husajiliwa kwa jeshi na baadaye kurejea kwa jamii
Published 07/19/21
katika Makala haya tunajikita  nchini Kenya ambapo mchakato mzima wa kufanyia katiba marekebisho umekwama kutokana na hatua ya mahakama kuu nchini humo kusimamisha mchakato huo  kwa msingi kuwa wanzilishi wa mchakato huo rais Uhuru Kenyatta, na kingozi wa upinzani Raila Odinga, hakufuata sheria wakati wakianzisha mchakato huo. Benson Wakoli amelizamia swala hili katika makala haya
Published 07/06/21
Tarehe 16 ya mwezi Juni kila mwaka Bara la Afrika linaadhimisha siku ya mtoto wa Afrika, lengo likiwa ni kuikumbusha jamii na mataifa ya Afrika kuhusu umuhimu wa kulinda na kutetea haki za watoto.  Mkataba wa haki  za watoto kwa mara ya kwanza uliridhiwa na uliokuwa umoja wa Afrika OAU Julai 11 mwaka 1990 na kuanza kutekelezwa tarehe 29 November mwaka 1999, baada ya miaka 25 toka mkataba huo kuridhiwa ambapo nchi 47 za Afrika zilitia saini mkataba huu.
Published 06/21/21
Katika makala haya tunajadili iwapo bara la Africa, limetambua umuhimu kuwa  huru, na iwapo bado mataifa ya magharibi yana ushawishi kwa siasa kwa mataifa Africa, na uchumi wake. Benson wakoli amezungumza na mwanahistoria Lugete Mussa Lugete.
Published 06/08/21
Hakuna taifa  lina uwezo wa kuwarejesha wakimbizi katika mataifa yao bila ya hiari yao, sheria za kimataifa zinawalinda wakimbizi, anavyoeleza wakili Ojwang Agina, katika makala haya.
Published 06/03/21
Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR, limeeleza kuguswa na visa vya  mamlaka nchini Tanzania, kuwazuia wakimbizi na watafuta hifadhi wanaokimbia mashambulizi ya wanajihadi eneo la Cabo Delgado nchini Musumbiji kuingia nchini Tanzania. Kwa mjibu wa UNHCR ni kwamba wakimbizi 1,500 walazimika kurejea katika eneo la mapigano hali ambayo imetajwa kuwa ya kusikitisha sana. Katika makala haya nitazungumza na wakili Ojwang Agina kutoka nchini Kenya mbaye anafafanua...
Published 05/24/21
Katika Makala ya Jua Haki Zao, juma hili tunaangazia hukumu ya kifo ambayo bado mataifa mengi duniani yanatelekeza hukumu hiyo, hapa tunajadili umuhimu wa maisha kwa mjibu wa maandiko matakatifu na sheria za kimataifa kuhusu hukumu hii ya kifo. Tangu mapema miaka ya 60, wanaharakati katika mataifa mbali tayari walikuwa wameanza harakati za kushinikiza kuondolewa kwa hukumu ya Kifo, wengi wakidai hukumu hiyo inakiuka haki ya kimsingi ya binadamu kuishi.
Published 05/11/21
Kwa mjibu wa shirika la umoja wa mataifa UN, msichana au mwanake moja kati ya 4 huwa amekeketwa kwa kutumia za njia za kiasili au hata wengine hukeketwa na watalaam wa afya wasiozingatia maadili. Madaktari na wanaharakati wanasisitiza katika makala haya ya juhudi zaidi kufanywa ili kukomesha ukeketaji, ambao bado baadhi ya jamii za kiafrica zinaendeleza, licha ya madhara yake kwa wanawake na wasichana
Published 05/03/21
Katika makala haya tunadali swala ukeketeji wa wanawake barani afrika, ambalo kwa mjibu wa shirika la afya dunia WHO, mataifa 29 katika bara hili bado ya wanakeketa wanawake licha ya hamishisho ambazo zimefanywa kwa jamii kuachana na mila hiyo ambayo imepitwa na wakati na mbayo ina mathara mengi ya kiafya kwa wanawake.
Published 04/26/21
Masharika ya kiraia nchini Kenya yanapinga hatua ya serikali kutangaza kufungwa kwa Kambi za wakimbizi za Kakuma na Dadaab, masharika hayo yakisema serikali inakikuka sheria sheria. Mwanshidhi wetu Benson Wakoli, amefanya mahojiano na James Cira, Kutoka Twaweza East Africa Kenya, kujua msimamo wa mashirika ya kiraia kuhusu kufungwa kwa kambi hizo.
Published 04/20/21
Serikali ya Kenya ilitoa makataa kwa shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNCHR ,kufunga kambi za wakimbizi ya Daadab na Kakuma kwa kohofu makali ya Corona na swala la usalama.Hata hivyo mashirika ya kiraia yalifika mahakamani kupinga hatua huyo. Peter Solomon ni mmoja wa wakenya waliofika mahakamani. Mwandishi wetu Benson Wakoli amefanya mahojiano naye,kufahamu ni kwa nini anapinga kufungwa kwa kambi hizo.
Published 04/20/21
Imetimia miaka 13 tangu bara la Afrika kuridhia tamko la demokrasia, utawala bora na chaguzi huru za haki. Tunaangazia tamko hilo na wajibu wa viongozi na asasi za kiraia kukuza demokrasia barani Afrika. Ungana na Fredrick Nwaka katika makala ya Jua haki zako akizungumza na Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC, Ana Henga
Published 02/04/20
Mara kadhaa katika mataifa ya Afrika kumeripotiwa matukio ya kuvunjika kwa uchumba baina ya mwanaume na mwanamke waliokuwa na matarajio ya kufunga ndoa. Je utaratibu wa kisheria ukoje? Ungana na Fredrick Nwaka katika makala ya Jua Haki Zako
Published 12/02/19