Episodes
Taarifa Muhimu kwa Makampuni yanayouza Soybean katika soko la China
Published 04/03/23
Taarifa kwa Watanzania wanaoishi China kuhusu tahadhari wanazopaswa kuchukua dhidi ya maambukizi ya UVIKO19
Published 12/11/22
Taarifa kuhusu bidhaa za uvuvi (wild aquatic products) zinazohitajika kwa wingi katika soko la China na utaratibu wa kujisajili ili kuuza China kufuatia mkataba uliosainiwa wakati wa Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk.Samia Suluhu Hassan nchini China
Published 12/05/22
Taarifa ya Balozi Mbelwa Kairuki kwa Waandishi wa Habari kuhusu maandalizi ya ziara ya Kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
Published 10/29/22
Ujumbe Maalum kwa wanafunzi watanzania wanaojiandaa kwenda Masomoni nchini China
Published 09/16/22
Taarifa kwa Umma Kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Ushirikiano wa Uchumi kati ya Tanzania na Jimbo la Zhejiang la nchini China. o la Zhejiang (CCPIT- Zhejiang Sub Council) Ndugu Chen Zongyao jijini Hangzhou. Zhejiang ni mojawapo ya Majimbo ya China yenye nguvu kubwa ya kiuchumi ikiwa na GDP ya Dola za Kimarekani Bilioni 849 na GDP per capital ya Dola za Kimarekani 14,907. Kutokana na utajiri wa Jimbo hilo, zipo fursa nyingi za biashara na uwekezaji.
Published 09/03/22
Taarifa kwa Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma katika Vyuo Vikuu nchini China
Published 08/22/22
Hivi karibuni Shirika letu la Ndege la Air Tanzania limetangaza kurejesha safari ya kwenda Guangzhou nchini China kuanzia tarehe 17 Julai 2022. Kufuatia tangazo hilo Ubalozi umepokea ujumbe kutoka kwa wananchi mbalimbali hususan wafanyabiashara wakitaka kujua kama hivi sasa China imefungua mipaka yake na kwamba watanzania wataweza sasa kuja China na Air Tanzania kwa ajili ya shughuli zao.
Published 07/10/22
Ujumbe kwa wafanyabiashara na waagizaji wa bidhaa kutoka China
Published 06/26/22
Balozi Kairuki aiomba Jumuiya ya kimataifa kushirikiana katika kulikabili janga la UVIKO19 badala ya kuyabagua mataifa ya Afrika yaliyoiwezesha dunia kufahamu aina mpya ya kirusi cha UVIKO19 (OMICRON). Rai ameitoa katika Mkutano wa Kimataifa wa Mwaka 2021 wa Imperial Springs uliofanyika jijini Guangzhou
Published 12/07/21
Taarifa muhimu kuhusu Ufadhili wa Masomo (Scholarships) China na changamoto kwa wanafunzi
Published 10/15/21
Mwongozo wa utaratibu wa kuuza muhogo mkavu katika soko la China kwa Makampuni ya Tanzania yenye nia ya kuchangamkia fursa ya soko
Published 10/15/21
Hotuba ya Balozi Mbelwa Kairuki katika Mkutano na Watanzania wanaofanya Biashara na Kuishi nchini China uliofanyika tarehe 8 Agosti 2021
Published 08/08/21
Ujumbe wa kuhamasisha kilimo cha Soybeans nchini Tanzania kwa ajili ya soko la China
Published 08/02/21
Taarifa kwa wadau wa Madini nchini kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Madini utakaofanyika jijini Tianjin tarehe 24 Oktoba 2021
Published 07/26/21
Kwa kutambua uhitaji wa Msaada wa kununua Mashine na mitambo ya uzalishaji kwa ajili ya kuanzisha viwanda vidogo, vya kati na vikubwa- kuanzia tarehe 1 Septemba Ubalozi wa Tanzania Nchini China utaanzisha DAWATI LA VIWANDA. Dawati hilo litatoa huduma kwa watanzania watakaokuwa na nia ya kununua kutoka China mitambo ya kuzalisha bidhaa mbalimbali nchini.
Published 07/06/21
Taarifa muhimu kwa Watanzania wanaosoma nchini China kwa ufadhili wa China Scholarship Council. Taarifa hiyo inatoa mrejesho kuhusu baadhi ya masuala ambayo wanafunzi waliyawasilisha katika Mkutano Mkuu wa Wanafunzi wanaosoma China uliofanyika tarehe 22 Mei 2021
Published 06/08/21
Mara nyingi Ubalozi unapotangaza fursa mpya ya soko- swali linaloulizwa na watu wengi ambao wanafikiria kuchangamkia fursa hiyo ni  "wananunua kwa bei gani au offer yao ni kiasi gani". Ni vizuri kuwa na ufahamu wa jumla kuhusu mwenendo wa bei ya soko la dunia la bidhaa hiyo. Hata hivyo ni muhimu zaidi kwa anayetaka kuuza bidhaa - awe ndio mtoa bei kwani mwenye mali ndio anajua gharama aliyoingia kuipata mali yake na ili asipate hasara anatakiwa kuuza kwa bei gani.Hivyo, unapojipanga kuuza...
Published 05/27/21
Taarifa ya kwa Umma kuhusu hafla ya kuonja kahawa ya Tanzania "Coffee Cupping" itakayofanyika jijini Changsha tarehe 14-18 Juni 2021. Hafla hiyo itakayohudhuriwa na Makampuni yanayonunua kahawa katika soko la China itawezesha wauzaji wa kahawa ya Tanzania kutangaza bidhaa yao katika soko la China
Published 05/06/21
Taarifa kwa umma inayohusu watanzania wanaosoma vyuo vikuu vya China ambao hivi sasa wapo Nje ya China kutokana na kufungwa mipaka ya China
Published 05/01/21
Watanzania wengi hununua bidhaa mbalimbali nchini China kwa madhumuni ya bishara na matumizi binafsi. Baadhi yao wamekumbwa na kadhia ya kuibiwa au kutapeliwa na wafanyabiashara wa kichina. Ujumbe huu unatoa ushauri wa mambo ya kuzingatia ili kuepuka kadhia inayoweza kutokea
Published 04/25/21