Episodes
Kotlin ndio lugha chagua kwa Google kwa kutengeneza mifumo katika program ya Android. Java huenda isiendee tumika na kupata usaidizi wa moja kwa moja toka Google hapo baadae.
Published 06/23/19
Kuwa Mtengeneza Mifumo Tanzania kunaambatana na changamoto na fursa mbalimbali. Katika toleo hili nitakurudisha enzi za zamani nakupata hadhithi za watengeneza mifumo wa zamani. Pia nitakusimulia niliaonza chuo changamoto nilizopitia na kupata kazi. Pia nimeainisha fursa zilizopo sasa kwa watengeza mifumo wa leo.
Published 05/26/19
Leo nitazungumza juu ya mambo nitayo fanya nikiwa kwenye mafunzo Mbeya.
Published 03/24/19
Ebwana mambo vipi, leo nitakupa taarifa ya kazi nilizofanya kwa wiki mbili.
Published 02/24/19
Leo tutaangalia kwa nini hupaswi achwa nyuma na hili joto la Machine Learning na kwa wepesi tuu ni vipi Machine Learning inafanya kazi. Kumbuka wiki iliyopita nllikupa chachu tuu ya Machine Learning na kama bado hujasikia toleo lililopita nakusihi sasa usikilize ili twende pamoja.
Published 02/04/19
Leo nitakupa chachu kidogo tuu kuhusu Machine Learning, nimejaribu kufuta maana yake kwa Kiswahili sijapata neno lililo rasmi juu ya Machine Learning. Ni imani yangu tutaelewana tuu hakuna tatizo kabisa, ndio Machine Learning.
Published 01/27/19
Leo tutazungumza namna ya kuweka vipaumbele kwenye kutengeneza mifumo ya kompyuta. Bila kuweka vipaumbele unaweza tengeneza mfumo usioisha au ambao watu hawata tumia. Hivi karibuni nimekutana na mambo mawili ambayo yamenisukuma andaa podcast toleo la leo. Kama utakuwa umenifollow kwenye mitandao ya kijamii basi unaweza kuwa umekutana na post nitazozungumza hapa.
Published 01/20/19
Leo tutazungumza wapi utaanzia tengeneza mifumo ya kompyuta, watu wengi wamekuwa wakiniuliza namna gani wanaweza anza tengeneza mifumo ya kompyuta au lugha gani nijifunze ipi ni bora kuliko nyingine. Na wengine hushangaa mambo ninayopost kwenye mitandao ya kijamii na kuuliza hivyo vinini unaweka, jibu linaweza kuwa rahisi kuwa ni Code. Lakini kwa mtu ambaye hayuko kwenye uwanja wa TEHAMA basi huwa natumia muda kidogo fafanua hili.
Published 01/06/19