Episodes
Wengi huitazama hisia ya Upweke kwa mtazamo hasi lakini episode hii itakufundisha namna ya kuitazama hisia kama fursa ya kutambua mahusiano sahihi kwako pamoja na mbinu ya kukabiliana na Upweke. Zaidi utajifunza kupitia maisha ya Education Specialist Remi ambaye alikabiliana na changamoto hii ya upweke.
Published 11/30/20
Published 11/30/20
Episode hii itakuongoza kupitia mwanasaikolojia mzoefu, namna gani ya kuikaribisha furaha kwenye maisha yako hata wakati wa changamoto. Huku ukijifunza mengi kuihusu furaha kutoka kwenye stori ya maisha ya mchekeshaji nguli JOL Master. 
Published 11/30/20
Maisha ni Milima na Mabonde na episode hii itakufundisha mbinu za kurudisha Matumaini pale unapoyapoteza na faida za kuishi kwa Matumaini kama anavyothibitisha Muanzilishi na Mkurugenzi wa Simulizi na Sauti (SnS), bwana Fredrick Bundala a.k.a Skywalker.
Published 10/22/20
Fahamu zaidi kutoka kwa mwanasaikolojia mzoefu kuhusu stress  na njia bora za kukabiliana nayo. Na kwa namna ya kipekee jinsi Stress ilivyogeuka kuwa Fursa na kubadilisha maisha Banker mzoefu, bwana Stephen Matinya.
Published 10/22/20
Kujihisi uko mahali sahihi ukifanya kitu sahihi kinachoendana na kusudi lako hapa duniani ni hisia iletayo Furaha timilifu na endelevu kwenye maisha. Sikiliza episode hii ujifunze mengi kuhusu Fulfilment na kwa kipekee kabisa jinsi ilivyoyagusa maisha ya Nguli wa Ubunifu wa Mitindo Tanzania, Khadija Mwanamboka.
Published 10/08/20
Hofu ni sawa na alarm ya mwili kwenye maisha, ikitoa taarifa za hatari na kukumbusha yale yalio muhimu zaidi. Sikiliza episode hii ufahamu zaidi kutoka kwa Mwanasaikolojia mzoefu ni kwa namna gani Hofu huifanya kazi hiyo ya alarm pamoja na mengine muhimu kuhusu hisia ya Hofu.
Published 10/08/20
Sikiliza kufahamu namna Emotional Intelligence invyoweza kuwa Baraka kubwa kwenye Ajir ama Biashara yako kupitia faida zake. Pia utapata muongozo kutoka kwa Mwanasaikolojia mzoefu wa namna gani unaweza kuitumia Emotional Intelligence kwa tija kwenye Ajira au Biashara yako.
Published 09/27/20
Fuatilia episode hii kujifunza kama mzazi unawezaje kuikaribisha Emotional Intelligence kwenye Familia yako na manufaa yake kwako na kwa familia ni yapi?
Published 09/27/20
Fahamu namna ambavyo unaweza kuitumia Emotional Intelligence kutatua changamoto mbalimbali kwenye mahusiano yako ya kimapenzi.
Published 09/12/20
Fahamu mbinu ya kujifanyia tathmini kihisia ili kujua vyanzo na masuluhisho ya changamoto mbalimbali unazopitia kihisia. 
Published 09/12/20
Fahamu kutoka kwa mwanasakolojia mzoefu kuhusu maana ya Akili Hisia (Emotional Intelligence), tofauti kati ya Emotions na Feelings, nguzo za kuijenga Akili Hisia pamoja na faida zake kwenye maisha yako.
Published 09/12/20