Episodes
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP nchini Sudan Kusini kupitia programu yake ya chakula shuleni imefanikiwa kuwasaidi wasichana wengi kuepukana na ndoa za utotoni.  Sudan Kusini ni moja kati ya mataifa yenye viwango vya chini vya watu wanaojua kusoma na kuandika hususani kwa wasichana. Jamii katika taifa hilo la afrika ya mashariki huwaoza mabinti ikiwa ni njia moja wapo ya familia kujipatia mali na hivyo mtoto wa kike hujikuta akikosa haki yake ya msingi ya kupata...
Published 04/05/24
Hii leo jaridani tunaangazia vita katika Ukanda wa Gaza ukielekea miezi siti hapo kesho, na programu ya mlo shuleni nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Rwanda na mashinani nchini DRC, kulikoni?”. Kesho kutwa jumapili ikiwa ndio itatimu miezi sita ya mzozo wa Gaza, huko Mashariki ya Kati, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo amezungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani akirejelea wito wake wa sitisho la mapigano kwa misinigi ya kiutu, kuachiliwa...
Published 04/05/24
Kesho kutwa jumapili ikiwa ndio itatimu miezi sita ya mzozo wa Gaza, huko Mashariki ya Kati, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo amezungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani akirejelea wito wake wa sitisho la mapigano kwa misinigi ya kiutu, kuachiliwa kwa mateka wote bila masharti, ulinzi wa raia na misaada ya kiutu ifikie walengwa bila vikwazo vyovyote huku akikgusia pia Israeli kutumia akili mnemba kwenye operesheni zake.  Guterres akianza hotuba yake...
Published 04/05/24
Lengo namba 5 la maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa au SDG5 linahimiza kila nchi kuhakikisha wanawake wanawezeshwa na kujumuishwa katika kila nyanja ya Maisha ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 hawasalii nyuma katika maendeleo. Moja ya masuala yanayotiliwa msukumo zaidi hivi sasa ni ujumuishwaji wa wanwake katika masuala ya huduma za kifedha n anchi nyingi zimeanza kuchukua hatua ikiwemo Tanzania. Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili amezungumza na Nangi Moses Massawe kutoka Benki Kuu...
Published 04/04/24
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adhuhuri na Alasiri.”
Published 04/04/24
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia ujumuishwaji wa wanawake katika masuala ya kifedha kwa lengo la kutimiza lengo la Umoja wa Mataifa la usawa wa kijinsia katika Nyanja zote. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na katika kujifunza kiswahili tunakuletea ufafanuzi na tofauti ya maneno “Adhuhuri na Alasiri”. Leo ni siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na msaada wa kuchukua hatua dhidi ya mabomu hayo. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mabomu,...
Published 04/04/24
Umoja wa Mataifa umekuwa ukipigia upatu lengo namba tano la Malengo Endelevu ya Umoja huo linalohimiza usawa kwa wote katika nyanja zote ifikapo mwaka 2030. Hata hivyo ili kuelewa jinsi biashara inavyoathiri wanaume na wanawake ni muhimu kuunda sera za biashara zinazojumuisha zaidi na zenye usawa ambazo zinakuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa kiuchumi kwa wote,hii inahitaji takwimu nzuri za kitaifa kuhusu jinsia katika biashara. Kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na...
Published 04/03/24
Siku zikizidi kuhesabiwa kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, kuondoka nchini humo, ujumbe huo unaendelea kutekeleza wajibu wake wa kujengea uwezo jeshi la serikali, FARDC kuweza kukabili vikundi vilivyojihami ambavyo vinatajwa kuhusika na asilimia 65 ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo mwezi Februari mwaka huu, kwa mujibu wa ripoti ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na serikali. Je, FARDC linajengewa uwezo gani?...
Published 04/03/24
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala inatupeleka nchini kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni? Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo kwa mara nyingine yameonya kwamba bila dalili zozote za usitishaji mapigano Gaza hali ya kibinadamu inaendelea kuwa janga huku mashambulizi ya Israel yakiendelea kukatili maisha, kufurusha watu na kusababisha uharibifu usioelezeka na njaa nayo...
Published 04/03/24
Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo kwa mara nyingine yameonya kwamba bila dalili zozote za usitishaji mapigano Gaza hali ya kibinadamu inaendelea kuwa janga huku mashambulizi ya Israel yakiendelea kukatili maisha, kufurusha watu na kusababisha uharibifu usioelezeka na njaa nayo ikiongeza hofu ya hatma ya watu wa eneo hilo.  Asante Anold kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA usiku wa kuamkia leo makombora ya Israel yameendelea...
Published 04/03/24
Kinara wa elimu nchini Tanzania Paulina Ngurumwa anasema bado kazi ipo kupigania haki za mwanamke kwa hiyo harakati hizo hazitakiwi kupoa. Paulina Ngurumwa ni mwanaharakati wa haki za kijamii kupitia shirika la KINNAPA Development Programme.  KINNAPA Development Programme ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa na wanajamii ya Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara, kaskazini mwa Tanzania likiwa ni chombo cha kutatua matatizo yao hasa ya ardhi. Shirika hili lilianzishwa mwaka 1992 na kwa...
Published 04/02/24
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika harakati za kuwainua wanawake na wasichana nchini Tanzania Tanzania, ambapo Paulina Ngurumwa kutoka KINNAPA Development Programme, shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa na wanajamii ya Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara anazungumza na Anold Kayanda wa idhaa hii. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani. Leo maafisa wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamelaani vikali mauaji ya wafanyakazi wa misaada 7 wa shirika...
Published 04/02/24
Maji ni uhai, ni kauli mbiu ya miaka nenda rudi, lakini imesalia ndoto kwa wengi duniani hasa wakati huu mabadiliko ya tabianchi yanachochea ukame unaovuruga maisha ya binadamu, wanyama na mimea. Nchini Kenya katika kaunti ya Wajir, iliyoko kaskazini-mashariki mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, uhaba wa maji ulisababisha familia kupoteza mifugo yao, mazao kukauka na ustawi wa jamii kutoweka. Lakini shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, kwa kushirikiana na serikali ya Kaunti...
Published 04/01/24
Mratibu Mkuu wa Misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths amesema shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA ni uti wa mgongo wa operesheni za Kibinadamu Gaza hivyo jaribio la kulitenga shirika hilo lazima likome.  Bwana Griffiths ametoa kauli hiyo leo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X zamani Twitter akisistiza kuwa juhudi zozote za kusambaza misaada ya kibindamu kwenye Ukanda wa Gaza bila kupitia shirika la...
Published 04/01/24
Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu Gaza, na jitihada za kukabili habari potofu nchini DR Congo. Makala tunaku[eleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni? Mratibu Mkuu wa Misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths amesema shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA ni uti wa mgongo wa operesheni za Kibinadamu Gaza hivyo jaribio la kulitenga shirika hilo lazima likome.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia...
Published 04/01/24
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kituo kilichojengwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO kimesaidia vijana kukabiliana na habari potofu na za uongo ambazo huchochea ukosefu wa amani kwenye taifa hilo la Maziwa Makuu barani Afrika.  Jean Claude Batumike, ambaye ni Mkuu wa kituo cha vijana cha Amani, kilichoko eneo la Kamanyola huko jimboni Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akizungumza kupitia video ya MONUSCO iliyochapishwa...
Published 04/01/24
Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 ulifunga pazia hivi majuzi jijini New York Marekani ukipigia chepuo uwekezaji kwa wanawake na wasichana, na leo tunabisha hodi nchini Kenya wasichana waliokumbwa na ujauzito utotoni na kukatishwa ndoto za kuendelea na masomo au kupata ajira wamepata jawabu la changamoto wanazokumbana nazo pindi wakijifungua watoto wao. Changamoto kama vile mahali pa kumwacha mtoto kwa malezi ili aweze kuendelea na shule au kupata ajira.  Umoja wa...
Published 03/28/24
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “UDENDA”.
Published 03/28/24
Hii leo jaridani tnakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kufuatilia jitihada za mashirika za kuhahikisha watoto waathrika wa mimba za utotoni wameweza kurejea shule. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za Gaza, Haiti na wakimbizi wakimbizi wa Sudan Kusini. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunapata maana ya neno “UDENDA.”  Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina (UNRWA) leo Machi 28 limetahadharisha kuhusu ujio wa baa la njaa katika Ukanda wa...
Published 03/28/24
Mgogoro ambao hauripotiwi sana kaskazini mwa Msumbiji umesababisha mamia kwa maelfu ya familia kuwa wakimbizi, ambao wanaendelea kutatizika kutafuta chakula, malazi na usalama. Anold Kayanda anasimulia zaidi katika makala hii.
Published 03/27/24
Mwanamuziki Innocent Balume, al maaruf Innoss’B ametangazwa kuwa muungaji mkono wa ngazi ya juu wa shirika la  Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP katika kusongesha milo yenye afya na lishe bora nchini mwake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Nimeshuhudia njaa mara nyingi sana wakati wa utoto wangu, kabla ya kwenda shule tulikuwa na njaa na kabla ya kulala tulikuwa na njaa, ndivyo asemavyo mwanamuziki Innocent Balume, al maaruf Innoss’B ambaye ametangazwa kuwa muungaji...
Published 03/27/24
Hii leo jaridani tunaangazia jitihada za kukomesha mlipuko wa kipindupindu uliozuka nchini Zambia, na mchango wa wasanii katika msaada wa kibinandamu nchini DRC. Makala tunamulika mgogoro ambao hauripotiwi sana kaskazini mwa Msumbiji na mashinani tunasalia nchini DRC, kulikoni? Juhudi na ushirikiano wa pamoja wa wahudumu wa afya, vituo na Jamii, vimefanikisha kukomesha mlipuko wa kipindupindu uliozuka nchini Zambia kwa mujibu wa Shirika Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO nchini Zambia,...
Published 03/27/24
Juhudi na ushirikiano wa pamoja wa wahudumu wa afya, vituo na Jamii, vimefanikisha kukomesha mlipuko wa kipindupindu uliozuka nchini Zambia kwa mujibu wa Shirika Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO nchini Zambia, ambalo limeeleza kwamba ugunduzi wa mapema na matibabu husaidia kukabiliana na ugonjwa huo na kupunguza idadi ya vifo.  Jioni moja Philta Samazimva alilalamika ghafla tumbo kuuma, baada ya kuharisha sana, mama yake mzazi Hildar Samazimba alimpeleka kliniki. Baadhi ya watu hapa...
Published 03/27/24
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DR Congo ambako Umoja wa Mataifa unasema wananchi milioni 23.4 wanakabiliwa na njaa. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu SEA, machafuko DRC na vifo vya wahamiaji. Mashinani inamulika miradi ya maji nchini Tanzania.  Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Hatua Maalum za Ulinzi dhidi ya Unyonyaji na Unyanyasaji wa Kingono imewekwa wazi hii leo.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia...
Published 03/26/24
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwakushirikiana na wadau wake wamefungua nyumba salama huko Andari Magharibi katika jimbo la Equatoria kwa ajili ya kusaidia manusura wa unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro nchini humo. Leah Mushi na maelezo zaidi. Kwa mujibu wa Mkuu wa zamani wa UNMISS ofisi ya Yambio, Christopher Muchiri Murenga, mradi huu ulioanzishwa na kitengo cha ushauri cha ulinzi wa wanawake cha UNMISS na umefadhiliwa na Muungano wa Ulaya pamoja na...
Published 03/25/24